Tuesday, June 11, 2013

USHAHIDI WA PICHA MWANA CHAMBER SQUARD NOORAH A.K.A BABA STARZ AFUNGA PINGU ZA MAISHA


Noorah akiwa na mke wake
umamosi ya June 8 ilikuwa ni ya kihistoria kwa muziki wa Tanzania kwakuwa pamoja na kutolewa tuzo za KTMA, wasanii wawili, Noorah na H.Baba walifungua ndoa na kuisaliti rasmi kambi maarufu mjini ya makapela.
 
Harusi ya Noorah ilifanyika mkoani kwao Shinyanga na ameuambia mtandao huu kuwa ilienda vizuri na kila mmoja alifurahi.

“Kwangu mimi kiukweli ni ya kihistoria sana kwasababu kila mtu alikuwa happy. Unajua shughuli kama hii ni ya watu wengu, shughuli ikiwa na watu wengi halafu watu wote wakafurahi inakupa faraja kubwa sana hata wewe mwenyewe,” amesema Noorah ambaye mke wake anaitwa Camilla. “Ndoa ni commitment, ndoa ni majukumu, ndo ni vitu kama hivyo sasa kama nimefika hatua ya kuweza kudiriki kuthubutu kitu kama hicho maana yake najiona kwamba nimekomaa vizuri.” 
Noorah akiwa amembeba mke wake

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...