Tuesday, June 11, 2013

MSANII WA BONGO MOVIE KASH AFARIKI DUNIA



Marehemu Jaji Khamisi (Kashi)
Msanii wa filamu nchini Jaji Khamis (Kashi)aliyewahi kutamba na michezo ya ITV enzi zile akiwa na wasanii kama Mzee Masinde,Samson na wengine katika mchezo wa Tamu chungu na mingine mingi Amefariki dunia jana katika hosptali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa,akizungumza na mtandao huu Rais wa Shirikisho la wasanii amesema kuwa tasnia yake bado inaendelea kukumbwa na majanga lakini amedai yote ni kazi ya mungu
Nae mzee Masinde ambaye alikuwa nae katika kundi moja akiwa kama kiongozi wake amesema Kashi ni msanii ambaye alikuwa mpiganaji na kwa hakika ni pigo kubwa katika tasnia yetu
Mungu ailaze roho ya marehemu Jaji Khamis (Kashi)
mahali pema pepponi Amini.

1 comment:

  1. JAMA KAFA KWELI HUYU MBONA SIJASKIA KTK NEWS!!

    ReplyDelete

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...