Monday, November 12, 2012

WANAWAKE NA WATOTO WAONGEZEKA KUWA OMBA OMBA JIJINI DAR.




Kutokana na kushamili kwa wimbi la omba omba wengi katika jiji la Dar es Salaam chanzo chake kimeonekana ni wanawake na watoto ndiyo wengi kama walivyonaswa na kamera ya Kajunason Blog. Wanawake hao hukaa pembezoni mwa barabara na kuwatuma watoto wao waende barabarani waombe na kuwaletea pesa. Pichani watoto wakisubiri foleni za kwenye mataa ya Fire/Kariakoo jiji Dar es Salaam.

Mtoto akiomba mara baada ya daladala kusimama.



Watoto wengine hukimbilia magari madogo.

Watoto wakikomaa kuomba.

Wengine nao wakikimbilia gari ili waombe.

Akina mama waliwa wamekaa pembeni ya barabara wakisubiri watoto wao wawaletee hela walizoomba.


Ni aibu ila hakuna jinsi.


Mama akimtoa mwanae barabarani mara baada ya kuona kamera imemuulika.

Akina mama wengine waliamua kuondoka eneo hilo mara baada ya kuona wanapigwa picha.

Watoto wakiwa wamekaa pembezoni mwa barabara wakisubiri magari, hali ambayo ni hatari sana. Serikali haina budi kuchukua hatua kazi kwa watu hawa ili kuweza kukomesha omba omba ambao kwa sasa wametanda pembezoni mwa barabara za jiji la Dar.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...