Monday, September 10, 2012

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 LATIKISA MKOANI SINGIDA‏


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Cirryl a.k.a Kamikazi akikamua jukwaani usiku wa kuamkia  leo ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Ni Kushangweka tu ndani ya viwanja vya Singida Motel usiku wa kuamkia leo
Rich Mavoco akiwaimbisha mashabiki wake waliofika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta usiku wa kuamkia leo ambapo wakazi wa mji huo wamejitokeza kwa wingi kuwashuhudia wasanii mbalimbali wanaotumbuiza.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Shillole akijimwaya mwaya jukwaa mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Singida (hawapo pichani),usiku wa kuamkia leo
Pichani juu na chini Sehemu ya Umati wa watu waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye viwanja vya Singida Motel ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea.
Pichani kati ni msanii wa bongofleva kutoka THT,Recho akiwa sambamba na dansaz wake jukwaani wakikamua vilivyo.
Baadhi ya wakazi wa Singida waliojitokeza kwa wingi usiku wa kuamkia leokwenye tamasha la Serengeti Fiesta wakishangilia jambo.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Mabeste na msanii mwenzake wakitumbuiza jukwaani usiku wa kuamkia leo
Pichani ni Ofisa Mahusiano wa kampuni Clouds Fm,Simalenga akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini,Mh Queen Mlozi pamoja na nduguze wakishuhudia tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Singida Motel,Mkoani Singida ambapo wakazi wa mji huo wameitikia wito wa kujitokeza kwa wingi kuwashuhudia wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya
Anaitwa Ben Paul mmoja wa wasanii mahiri wa Bongofleva katika miondoko ya R&B
Shillole akiwapa dole mashabiki wake waliokuwa wakimshangilia kwa nguvu.
Pichani kulia ni Dj Zero akiwa amepozi mtangazaji wa kipindi cha XXL,wote wafanyakazi wa Clouds FM wakishoo love usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya viwanja vya Singida Motel.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...