Monday, September 17, 2012

MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI YANAYODHAMINIWA NA AIRTEL KUANZA LEO


Kamanda Mkuu Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga (kushoto) akipokea T-shirt kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde zitakazotumika katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani inayofanyika kitaifa mkoni Iringa ambapo Airtel ni wadhamini wakuu. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za makao makuu ya polisi usalama barabarni jijini Dar es Saalam. Anayeshuhudia ni Mkaguzi msaidizi wa polisi, Inspector Deus Sokoni, madhimisho ya wiki ya Usalama barabarani yanaanza leo Jumatatu.

Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akizungumza na maofisa wa polisi mara baada ya kukabidhi T-shirt ambazo zimebeba ujumbe usemao “Pambana na ajali za barabarani kwa vitendo, zingatia sheria” zitakazotumika katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani nchini nzima. Kulia ni Kamanda Mkuu Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga akifuatiwa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Inspector Deus Sokoni na kushoto ni Mratibu Msaidizi wa Polisi, Bonaventura Nsokolo.
Mfanyakazi wa Airtel, bwana Gregory Ndenyishau akishusha box lenye T-shirts ambazo zitatumika katika wiki ya usalama barabarani katika ofisi za makoa makuu ya polisi wa usalama barabarani jijini Dar es Saalam ambapo Airtel ni wadhamini wakuu wa kampeni ya usalama barabarni kwa mwaka huu, anayepokea ni Mratibu Msaidizi wa Polisi, Bonaventura Nsokolo.



No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...