Monday, September 17, 2012

KAMATI YA REDD’S MISS TANZANIA KUTEMBELEA KAMBI YA MISS TEMEKE 2012 LEO


Warembo wanaowania taji la Redd’s Miss Temeke 2012 wakiwa mazoezini jana kwenye Club ya TCC Chang’ombe. Shindano hilo litafanyika Ijumaa hii Sept 21, kwenye ukumbi wa PTA (Sabasaba Hall).



Warembo wanaowania taji la Redd’s litakalofanyika Ijumaa hii Sept 21, kwenye ukumbi wa PTA (Sabasaba Hall), wakiwasiliza wakufunzi wao kutoka kulia Joyce Maweda, Leyla Bhanji, Hawa Ismail na Mwajabu Juma wakati wa mazoezi yao jana kwenye Club ya TCC Chang’ombe.(Picha Intellectuals Communications Limited).
KAMATI ya Redd’s Miss Tanzania leo inatarajiwa kutembelea kambi ya Redd’s Miss Temeke 2012, kubwa ni kuwafunda vimwana hao kutoka Vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang’ombe, kuhusu mambo mbalimbali ndani ya mashindano ya urembo.
Kamati hiyo itaongozwa na Mkurugenzi wake, Hashim Lundenga atakayefuatana na mshauri wa masuala ya urembo katika kamati yao, Dk. Ramesh Shah, Katibu Bosco Majaliwa, Mkuu wa Itifaki, Albert Makoye na Mjumbe wa Kamati hiyo, Lucas Rutta.
Shindano la Redd’s Miss Temeke 2012, linafanyika Ijumaa hii katika ukumbi wa PTA (SabaSaba Hall) na tiketi za VIP zimeshaanza kuuzwa katika Club za City Sports Lounge iliyopo makutano ya Samora na Azikiwe na Nyumbani Lounge iliyopo maeneo ya Namanga ambapo VIP kwa mtu mmoja ni Tshs 50,000 na pia waweza nunua kwa meza moja ama ya watu 8 kwa laki 4 au watu kumi laki 5.


Mbali ya vinywaji vya Redd’s na Dodoma Wine, Miss Temeke pia imedhaminiwa na Global Publishers, Gazeti la Jambo Leo, katejoshy.blogspot.com, Mariedo Boutique, Push Mobile, City Sports Lounge, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders na 88.4 Cloud’s FM.
Shindano hili litakuwa ni miongoni mwa mashindano ya lala salama kabla ya kupata warembo watakaoungana na warembo wa kanda nyingine kuingia kambini kumtafuta mrembo wa Redd’s Miss Tanzania kwa mwaka huu.






No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...