Wednesday, August 8, 2012

ZAMARADI ADAIWA KUCHOCHEA BIFU LA NAY WA MITEGO NA SINTA

Mtangazaji wa kipindi cha Hatua Tatu Sintah akiwa kwenye pozi la aina yake.
 
MTANGAZAJI wa kipindi cha Take One, kinachorushwa hewani kupitia runinga ya Clouds TV, Zamaradi Mketema, anadaiwa kupika bifu la msanii wa filamu na Mtangazaji wa kituo cha Times Fm, Christina Manongi 'Sintah' a.k.a JLO Africa, na Mwanabongo Fleva Mbishi Nay wa Miteg, baada ya jana kurusha kipidi chake kilichokuwa  na mahojiano baina yake na  Nay wa Mitego, ambaye hivikaribuni ameachia single yake yenye  ujumbe wa kuwakejeri baadhi ya wasanii wa Bongo Movie.
Kufuatia mahojiano hayo kuwagusa wasanii wengi akiwemo Sintah, amening'iniza ujumbe mzito kwenye web site yake uliokuwa ukimponda Nay wa Mitego na Zamaradi,Ujumbe huo  pia umetolewa maoni kibao na wadau wa saiti hiyo ukilenga kumkejeri  kwa kumtusi Zamaradi na Nay wa Mitego, jambo linaloashiria hatari kubwa baina ya Sinta na Ney mara watakapokutana uso kwa uso.
Naomba niishie hapa kama hujaelewa ninachokisema ingia www.sintah.com uone ninachomanisha.

 
Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Bongo, Nay wa Mitego katika pozi

Mtangazaji wa kipindi cha Take One, Zamaradi Mketema akiwa katika pozi.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...