Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi kikombe Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Fatuma Salum Ally, baada ya Halmashauri ya Wilaya hiyo kuwa kuwa mshindi wa jumla katika maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika Agosti 8, 2012 mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mmoja kati ya wajasiliamali wa vikundi vya wakulima, wakati alipokuwa akifunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili wakati walipowasili kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma, kwa ajili ya kufunga rasmi maonyesho hayo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipomwakilisha Rais Jakaya Kikwete, kufunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Nanenane yaliyomalizika Agosti 8, 2012 katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha Tuzo aliyokabidhiwa kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa Rais katika kusimamia na kuendeleza Kilimo Kwanza, wakati Makamu alipokuwa akifunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma, Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza.
No comments:
Post a Comment