Wednesday, August 8, 2012

MTUNISI AANGUA KILIO BAADA YA KUKAMATA WEZI WA KAZI ZA FILAMU BONGO

Msanii wa filamu Bongo, Mtunisi akiangua kilio mbele ya mashabiki zake waliokuwa wakimtazama  baada ya kuwabaini wezi wa kazi zao.
 
KAMPUNI ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam inayosambaza kazi za wasanii kwa kushirikiana na wasanii wamekamata kazi mbalimbali za wasanii hawo zinazorudifiwa kinyume na taratibu na kutofaidika kwa wasanii wanaotoa kazi hizo

Msemaji wa Kampuni ya Steps Kambarage Ignatios amesema kuwa ukamataji huo si wa zimamoto watahakikisha wanashirikiana na wasanii wenyewe kukamata kazi zao maana wasanii wengi wanadai kuwa kazi zao zinatoka sana kumbe zinachakachuliwa na kuwapa faida watu ambao wanakaa tu na kusubiri kazi za wasanii ili waweze kujitengenezea faida bila jasho, ameiomba serikali kuchukua hatua kali ili iwe fundisho kwa watu wanaorudufu na kunyonya kazi za wasanii hawo


Mmoja wa wasanii waliojitokeza katika kamatakamata hiyo iliyofanyika makutano ya mtaa wa Magila na Likoma Kariakoo, Msanii Mohamedi Nice 'Mtunisi' amesema watu hawa wana akili za ziada kwani katika kava ya mbele wanaweka stika yetu halali na Dvd ndiyo inakuwa imechakachuliwa huku akiangua kilio na kusema wasanii wakifa wanakufa masikini kumbe ni watu wachache ndio wamekuwa wakinufaika na kazi zao bila kushiriki chochote


Baadhi ya wasanii walioshiliki katika kamata kamata hiyo ni pamoja na Jacobo Stevin 'JB' Mzee Yusuph wa kundi la Taarabu la Jahazi Simoni Mwapagata (Rado) Mussa Msuba wa iliyokuwa Segere Orginal Seles Mapunda ,Mohamed Nice 'Mtunisi' na wengine wengi wasanii hao wameungana pamoja kwa ajili ya kutetea kazi zao ili zisirudufiwe kiholela na kuiomba serikali kupitisha sheria kali kwa mtu anayekamatwa na kazi feki za wasanii


Baadhi ya wasanii  na askari polisi wakiwa wamezingira duka lililokuwa linauza filamu feki

Msanii wa filamu nchini Mohamed Nice 'Mtunisi' kushoto na Jacob Steven 'JB' wakiwa katika duka ambalo  linauza kazi zao  feki.

Maboksi ya kazi mbalimbali za wasanii zilizokamatwa.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...