Mshambuliaji mpya wa Timu ya Simba SC, Mrisho Ngassa akiwa mbele ya mkoko wake aliyopewa kama moja ya makubaliano na timu hiyo kwenye mkataba wake.
Kipa wa Timu ya Simba SC, Juma Kaseja akiongozana na Ngassa kuelekea mazoezini mapema leo.
THAMANI ya Mrisho Khalfan Ngassa katika klabu yake mpya, Simba SC kwa mujibu wa Mkataba aliosaini jana ni Sh. Milioni 30, kwa mwaka mbali na mishahara na marupurupu mengine.
Simba
ilifanikiwa kumalizana na Ngassa jana na kusaini naye mkataba wa miaka
miwili, ambao umemfanya aondoke na zaidi ya Sh. Milioni 35, Milioni 12
akipewa taslimu na nyingine akipewa gari.
Katika
mkataba huo wa Simba na Ngassa, mshambuliaji huyo atakuwa akilipwa Sh.
Milioni 2 mshahara kwa mwezi, Milioni 1 ipo kwenye fomu ya mkataba na
Milioni 1 atakuwa akiongezewa na mtu.
Usajili
wa mchezaji huyo, ulikakamilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya
Simba SC, Hans Pop, ambaye ndiye alitoa fedha hizo na baada ya
kumsainisha na kumkabidhi haki yake, ili kumuondolea usumbufu
akambadilishia ‘chipu’ ya simu, ili akina Seif Magari wasimpate.
Juzi
Simba ilimnunua Ngassa kutoka Azam kwa Sh. Milioni 25, lakini mchezaji
huyo wa zamani wa Yanga akagoma kwa sababu hakushirikishwa katika dili
hilo.
Kwa
kumuongeza ‘kifurushi’ cha Sh. Milioni 35, ina maana Simba imemsajili
Ngassa kwa Sh. Milioni 60 kwa miaka miwili, ambalo ni dau kubwa zaidi la
usajili kwa mchezaji huyo tangu aanze kucheza soka.
Yanga
ilimsaini kwa Sh. Milioni 25 jumla kutoka Kagera Sugar mwaka 2007
pamoja na uhamisho wake akasaini mkataba wa miaka mitatu, wakati miaka
miwili iliyopita, Azam ilimsajili kwa Sh. Milioni 55 pamoja na uhamisho
wake (Sh. Milioni 30) ikimsainisha mkataba wa miaka mitatu, ambao
ulitarajiwa kumalizika mwakani.
Azam
ilifikia uamuzi wa kumuuza Ngassa, baada ya mchezaji huyo iliyemsajili
kutoka Yanga miaka miwili iliyopita, kubusu jezi ya Yanga baada ya
kufunga bao la pili katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki
na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo (DRC).
Na
uamuzi huo, ni wa mzee Said Salim Bakhresa mwenyewe, ambaye alikerwa na
kitendo hicho akawaagiza wanawe, Wakurugenzi wa bodi ya timu wamuuze
mchezaji huyo popote, haraka iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment