Monday, August 27, 2012

FUNGA KAZI YA SERENGETI FIESTA 2012 ILIVYOFANA NDANI YA VIWANJA VYA TANGAMANO, TANGA

Mambo ya Fiesta Serengeti 2012 ndani ya Jiji La Tanga.

Show Love.

Mkuu wa vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga akitoa maelezo machache kwa Mtangazaji Millard Ayo wakati wakirusha matangazo live ndani ya Tanga.

The Dream Team ya Clouds Fm.

Mtangazaji Millard Ayo akifanya mahojiano na Sam Baruti.

Mtangazaji Millard Ayo akiongea na wakazi wa Tanga.

Mwanadada Loveness Love akiongea machache na wakazi wa Tanga.

wakazi wa Tanga walijishindia zawadi mbali mbali ikiwemo t-shirt na tiketi za bure.

Kwenye moja na mbili toka ndani ya viwanja vya Tangamano.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego pichani kati mwenye kipaza sauti akisoma namba za washindi waliojinyakulia piki piki mbili zilizotolewa na kampuni ya Push Mobile, wa tatu kulia ni Meneja Masoko wa kampuni ya Push Mobile,Rugambo Rodney na mwisho kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga,na nyuma kabisa ni Mkurugenzi wa utafiti Clouds Media Group, Ruge Mutahaba pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,Ephrahim Mafuru wakishuhudia tukio hilo usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Mkwakwani ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linafanyika.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group, Joseph Kusaga usiku huu mara baada ya kuwataja washindi waliojishindia piki piki mara baada ya kuchezeshwa bahati nasibu,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea,pichani kati ni Afisa Mahusiano wa Clouds Media Group, Simon Simalenga.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nuru akitumbuiza jukwaani usiku wa kuamkia leona shabiki wake mbele ya wakazi wa jiji la Tanga wanaondelea kutiririka ndani ya uwanja wa Mkwakwani ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

Msanii kutoka THT,ajae kwa kasi katika anga ya muziki wa bongofleva aitwaye Rachel akiimba jukwaani usiku wa kuamkia leo.

Pichani shoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Ephrahim Mafuru, Mkuu wa Vipindi Clouds FM,Sebastian Maganga sambamba na Meneja wa bia ya Serengeti,Allan Chonjo wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya uwanja wa Mkwakwani wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea kurindima.

Dj Zero kutoka Clouds FM akikamua.

Sehemu ya umati wa wakazi wa Tanga wakifuatilia kwa makini makamuzi ya Fiesta usiku wa kuamkia leo.





Moja ya zao la Supa Nyota kutoka Mkoani Mbeya akiimba jukwaani.



No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...