Monday, January 16, 2012

TAMASHA LA FAMILY DAY BONANZA LAWAVUTA TIP TOP CONNECTION, TOT NA MSONDONGOMA DAR LIVE MBAGALA

Kiongozi wa kundi la TIP TOP Connection Ahmed Ally ‘Madee’ akitumbuiza.

Malkia wa Mipasho Bongo, Khadija Omar ‘Khadija Kopa’, akichukua “vijisenti” kutoka kwa mashabiki wake waliokuwa wakimtunza.



Wanamuziki wa Msondo Ngoma, Hassan Moshi ‘TX Junior’ (kushoto), Maalim Gurumo na Shabani Dede , wakishabulia jukwaa.




Kundi zima la TIP TOP Connection likiwajibika jukwaani.

Mnenguaji wa TOT, Halima Said ‘Queen Emmy’, akionyesha ukali wake wa nyonga.
Mashabiki wakicheza kwa staili yao.

Mwanamuziki wa Bendi ya Msondo Ngoma, Shabani Dede, akiwajibika.
Malkia wa Mipasho Bongo, Khadija Omar ‘Khadija Kopa’, akionyoosha kidole juu ikiwa ni ishara ya mipasho.
Watoto waliofika ukumbini hapo wakishindana kucheza kiduku.
Wasanii wa kundi la JNY Unit wakifanya kweli.
Mnenguaji wa nyimbo za Kikongo, King Jobiso, akitetemesha mashabiki.
Baadhi ya umati wa mashabiki waliofika katika uwanja huo wa burudani.
Watoto wakijinafasi kwa kuogelea.
Watoto wakifurahia “kusafiri kwa treni” katika kituo hicho cha burudani.
Kikundi cha nyimbo za asili cha Art Group, kikikamua.
Watoto wakiogelea kwa kutumbia mitumbwi ya plastiki.




KUNDI la Tip Top Connection la Manzese jijini Dar es Salaam, Bendi ya Msondo Ngoma na kundi la Tanzania One Theater ‘TOT’ lililo chini ya malkia wa mipasho Bongo, Khadija Kopa, jana waling’ara vilivyo katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam, katika shoo zao za kwanza kufanyikia ndani ya ukumbi huo wa mashabiki kibao.


Shoo hiyo iliyokuwa imefurika umati wa wasaka burudani tangu mishale ya saa tano asubuhi ilijumuisha ngoma za asili na wasnii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Mbagala walioonyesha umahiri wao bila ajzi.

Msondo Ngoma ndiyo ilianza na ikafuatiwa na TOT ambapo pazia lilifungwa na TIP TOP Connection.



No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...