Monday, January 16, 2012

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA YA KUNUNUA MAFUTA KWA NJIA YA AIRTEL MONEY KATIKA VITUO VYA GAPCO





Meneja uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Bw Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma ya kununua mafuta ya gari na ya taa kupitia huduma salama, rahisi na ya haraka ya Airtel money jijini Dar-es-Salaam jinsi wanavyoweza kufaidika na huduma hiyo ambayo itawarahisishia maisha ya kila siku kuepuka kutembea na pesa nyingi mifukoni lakini wakiwa na huduma hiyo wanaweza kuepuka usumbufu huo . Uzinduzi rasmi wa kununua mafuta kwa kutumia Airtel Money katika vituo vya Gapco Dar es Salaam umefanyika mwishoni mwa wiki.





Mteja wa Airtel Money, Bw David Ramadhani akitumia simu yake ya Airtel kununua mafuta ya gari kwa kutumia huduma ya Airtel Money katika kituo cha Gapco jijini Dar-es-Salaam. Anaemuwekea mafuta ni mhudumu wa kituo hicho, Bi. Nina Owiso na wa kwanza kushoto ni Mercy Nyange Afisa Uendeshaji wa Airtel Money akishuhudia mara baada ya hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo ya kununua mafuta kwa kutumia Airtel Money katika vituo vya Gapco Dar es Salaam iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Wafanyakazi wa Airtel wakishuhudi risti ya Airtel Money baada ya kutumia huduma hiyo kununua mafuta ya gari katika kituo cha Gapco jijini Dar-es-Salaam, kutoka kushoto ni Meneja Uendeshaji wa huduma ya Airtel Money, Bw. Asupya Nalingigwe, wa pili kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Bw Jackson Mmbando, kutoka kulia ni Meneja mauzo wa huduma ya Airtel Money, Bw John Ndunguru, wa pili kulia ni Mteja wa Airtel akishuhudia risiti hiyo na wa tatu ni Afisa Uendeshaji wa huduma ya Airtel Money akionyesha jinsi huduma ya Airtel Money inavyoweza kutumika katika ununuzi wa mafuta.

------

Airtel yazindua rasmi huduma ya kununua mafuta ya gari kwa Airtel Money katika vituo vya Gapco
Dar es salaam Tarehe 15, 2012

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mwishoni mwa wiki imezindua rasmi huduma yake mpya itakayowawezesha wateja kununua na kujaza mafuta kwenye magari yao katika vituo vya Gapco kwa kutumia huduma yao mpya ya Airtel Money, jijini Dare Salaam.

Akiongea wakati wa kuvitangaza vituo vitakavyotoa huduma hio kwa sasa jijini Dar es alaam kwa waandishi wa Habari, Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema "Lengo letu Airtel kupitia Airtel Money ni kuhakikisha huduma hii ya Airtel Money inakuwa suluhisho la kudumu kwa mahitaji ya kila siku kwa wananchi wote na wateja wetu kwa ujumla,
sasa unaweza kupata huduma katika vituo vya Gapco Dar es salaam pale Sasa Kazi-Mtoni Mtongani, Gapco Banana-Gongo la Mboto, na Gapco-bara bara ya Samora.

Lengo letu baada ya miezi miwili ijayo tuwe tumesambaza huduma hii ya kununua mafuta kwa Airtel Money katika kwa vituo vingi zaidi na watoa huduma hii wote!" Aliongeza kusema Mmbando.

Mbali na kutoa huduma ya kununua Mafuta kwa Airtel money vituo hivi pia ni Wakala wetu ambao pia mteja ataweza kutoa au kutuma fedha wakati wote vituo hivi vinapokuwa wazi.

Meneja Mauzo wa GAPCO, Mr Ben Temu alisema "huduma ya kununua mafuta ni rahisi kupitia Airtel Money, Wateja wote wa Airtel tunawakaribisha katika vituo vyetu vya Sasa Kazi- Mtoni Mtongani, Banana-Gongo la Mboto na kile cha Bara bara ya Samora mjinunulie mafuta kwa kupitia Airtel Money aliongeza kwa kusema " Ninaipongeza sana Airtel kwa kuja na huduma hizi bora zinazoonyesha ubunifu wa hali ya juu sasa hii inatupunguzia hatari ya kutembea na kiasi kikubwa cha pesa kadhalika hata wamiliki au wafanyabiashara wa petrol na disel kama sisi" alisema Mr Temu


Meneja uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Bw Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma ya kununua mafuta ya gari na ya taa kupitia huduma salama, rahisi na ya haraka ya Airtel money jijini Dar-es-Salaam jinsi wanavyoweza kufaidika na huduma hiyo ambayo itawarahisishia maisha ya kila siku kuepuka kutembea na pesa nyingi mifukoni lakini wakiwa na huduma hiyo wanaweza kuepuka usumbufu huo . Uzinduzi rasmi wa kununua mafuta kwa kutumia Airtel Money katika vituo vya Gapco Dar es Salaam umefanyika mwishoni mwa wiki.…

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...