Monday, August 15, 2016

BAADA YA TAARIFA YA MANJI KUJIUZULU, WANAYANGA WATIKISIKAMapema leo kuliibuka taarifa kuwa Yanga inaweza kumpoteza mwenyekiti wake Yusuf Manji ambaye inadaiwa kuwa anataka kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kusitisha kusudio lake la kuichukua na kuendesha kibiashara timu ya Yanga na nembo yake.
  
Habari hiyo imekuwa ikisambaa kwa kasi katika mitandao mbalimbali na mmoja wa viongozi wa Yanga alikiri kuwa suala hilo lipo.

Licha ya taarifa hizo kusambaa kwa kasi bado hakuna taarifa rasmi kuwa kiongozi huyo amechukua uamuzi huo zaidi ya tetesi.

Kwa mujibu wa mtandao wa salehjembe.blogspot.com, Manji amenuukuliwa akisema kuwa anataka aachwe na hataki kujibu hoja hiyo kama kweli amejiuzulu au la.

Baada ya taarifa hiyo kuendea Wanayanga wengi wamekuwa na maoni tofauti wapo wanaolalamika kuwa Manji ni mkombozi wao hasa katika masuala ya fedha na wengine wanadai anaweza kuondoka tu kwa kuwa msaada wake umefikia ukomo. Mjadala unaendelea.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...