Wednesday, February 3, 2016

YANGA WACHOMOKA KWA TAAABU MIKONONI MWA PRISONS YA MBEYA

 Baadhi ya wachezaji wa timu ya Yanga SC, wakizuia mpira wa adhabu uliokuwa ukipigwa kuelekea kwenye lango lao na mmoja wa wachezaji wa timu ya Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye mchezo wao wa ligi kuu Tanzania Bara ambapo timu hizo zilitoshana nguvu ya kufungana mabao 2-2.
Mchezaji wa Kimataifa wa Yanga Vicent Bosou kulia, akiongea jambo na mwamuzi wa mchezo huo.
KUFUATIA mchezo wa wikiendi iliyopita timu ya  Yanga SC, kujikuta iking'ang'aniwa kwa kupigwa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Coastal Union ya Tanga,  jana pia wamebanwa sero kwa kutoka sare ya kufungana 2-2 na timu ya Tanzania Prisons ya mkoani Mbeya kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Yanga walikuwa wakwanza kupata goli la kuongoza kupitia kwa Amis Tambwe dakika ya 35 akiunganisha krosi iliyopigwa na Haruna Niyonzima lakini bao hilo lilisawazishwa na Jeremia Juma Mgunda dakika ya 40 akimalizia krosi ya Mohamed Mkopi.
Mohamed Mkopi aliiandikia Prisons bao loa pili dakika ya 62 kipindi cha pili akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na kiungo wa zamani wa Yanga Juma Seif Kijiko.
Simon Msuva aliiokoa Yanga kwenye janga la kuchezea kichapo baada ya kuisawazishia Yanga kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Prisons Meshack Suleimani kuunawa mpira kwenye eneo la hatari kisha mwamuzi kuamuru upigwe mkwaju wa penati ambao ulikwamishwa wavuni ya Simon Msuva.


Yanga bado wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na pointi 40 huku tayari wamecheza mechi 17 wakifatiwa na Azam FC wenye pointi 39 sawa na Simba lakini Azam wao wanafaida ya michezo miwili mkononi wakiwa hawajacheza mechi hizo kutokana na kushiriki mashindano ya kirafiki nchini Zambia.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...