Wednesday, February 17, 2016

SIMBACHAWANE AWAPIGA CHINI WAKURUGENZI WANNE WA HALIMASHAURI!

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,George Simbachawane.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawane amewasimamisha kazi wakurugenzi wa nne kwa tuhuma za kuwahonga wakaguzi wa fedha kutoka katika ofisi ya Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) ili wapewe hati safi huku Halmashauri hizi zikiwa na ufisadi .

Wakurugenzi waliosimamishwa kazi ni Elizabeth Chitundu wa Halmashauri za Misenyi mkaoni Kagera, Ally Kisengi wa Halmashauri ya Nanyumbu mkaoni Mtwara na Abdalla Mfaume wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita.

Pia,Waziri Simbachawene amemsimamisha kazi mkurugenzi Halmashauri ya Tunduma Mkoani Mbeya Bi Halima Ajali ili kupisha uchunguzi kutokana matumizi mabaya ya madaraka ikiwa ni pamoja na kuwatumia watoto wake katika shuguli za halmashauri na kuwalipa posho na kusababisha upotevu wa mapato.

Aidha, Waziri Simbachawane pia ameziagiza mamlaka husika kuwasimisha kazi watendaji wa ofisi ya mkaguzi wa Hesabu za Serikali nchini,CAG waliohusika kupokea rushwa kutoka kwa wakurugenzi hao ili watoe hati safi kwenye Halmashauri hizo huku zikiwa na ubadilifu wa fedha za Umma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana Jijini Dar es Salaam,Waziri Simbachawene amesema Wakurugenzi hao wamegundulika baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na wizara yake

Akibainisha makosa ya kila mkurugenzi,Waziri Simbachawene amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misenyi, Bi Chitundu alimwagiza mweka hazina wake Majaliwa Bikwato atoe rushwa ya Milioni tatu kwa maafisa wa ofisi ya CAG kwa lengo la kuficha kasoro walizoziabini katika ukaguzi huo huku akijua ni kosa kisheria. Watumishi wa wa ofisi ya CAG waliopokea pesa hizo ni Stevin Buawa,John Elias pamoja na Kilembi Mkole

Katika Halmashauri ya Nanyumbu, Simbachawene amesema kuwa tarehe 26 Juni 2015, mkurugenzi wake bwana Kasengi pamoja na mweka hazina Pasco Malowo na mwasibu Emmanuel Mugesa walimkabidhi fedha Milioni 3 na laki tano afisa wa ofisi ya CAG kwa lengo la kutoa hati safi

Waziri Simbachawene amesema mwezi Novemba mwaka jana , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita Abdalla Mfaume na mweka hazina wake waliwapatia milioni 16 maafisa wakaguzi wa ofisi ya CAG ili wafiche ufisadi walioubaini

Amesema katika Halmashauri hiyo pia kumegundulika kuwepo na ufisadi mkubwa ikiwemo malipo ya mishahara hewa pamoja na malipo ya milioni 200 yaliotolewa pasipo kuwa na Stakabadhi

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...