Wednesday, February 17, 2016

MICHAEL OLUNGA APATA TIMU ULAYA, NI BAADA YA KUKOSA NAFASI KKATIKA CLUB YA ARSENAL!

Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Gori Mahia ya Kenya Michael Olunga.

Mchezaji wa timu ya Gori Mahia ya Kenya ambaye kwa muda mrefu alikuwa na ndoto za kuchezea timu ya Arsenal ya England, hatimaye ameamua kutimkia nchini  Sweden ambako amesaini mkataba wa miaka minne na klabu ya Djurgardens baada ya kukwama kupatiwa nafasi ya kujiunga na timu ya Arsenal.

Michael Olunga mwenye umri wa miaka 21 mwaka jana mwezi wa 8 alitengeneza video na kumuomba meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ili ampatie nafasi ya  kumsajili kutoka kwenye klabu yake ya Gor Mahia ya Kenya lakini ikashindikana na kuamua kubadili gia yake na kutimukia nchini Sweden ambapo amefanikiwa kuingia kadarasi ya miaka minne.

Akizungumza mmoja wa wasimamizi wake alisema kuwa Olunga amekuwa mtu mwenye ndoto za kufika mbali kisoka hivyo kila kukicha amekuwa akijituma kadri ya uwezo wake na kwa namna hiyo siku moja atakuja kutimiza ndoto zake za kuichezea hata klabu ya Arsenal.

“Anajitahidi sana, anajifunza kwa malengo mara zote anataka kujifunza ili kupiga hatua”, Mkurugenzi wa michezo Bosse Andersson alisema.

“Kwa maendeleo na mazingira yetu rafiki na yenye utulivu ya Djurgardens atajifunza na atakuwa bonge la Straika atakayeweza kucheza katika ligi kubwa Ulaya.

Hayo ndiyo matarajio ya Michael na anayosifa ya kufanya hivyo.

Olunga ambaye jina lake la utanini ‘Engineer’ kwa maana mhandisi kutokana na kuwa na Degree ya Uhandisi amesema anatambua kuwa itakuwa vigumu kuzoea mazingira haraka.

“Mwanzoni itabidi nijaribu kwenda lakini nikishazoea basi nitaendelea kufunga zaidi na zaidi. Aliiambiatovutiyaklabuhiyo”.

“Mpaka sasa nimeshacheza mechi za kirafiki tu lakini najiona ni povizuri”.

“Kila kitu kimeandaliwa vizuri uwanja wa kufanyia mazoezi upo safi, unaonekana kama upotayari kwakuchezea ligi kubwabarani Ulaya”.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...