Monday, February 15, 2016

SIMANZI MWANAMUZIKI JOHN WOKA AFARIKI DUNIA!

12728950_1436785056335908_7684240396242112615_n
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Michael Dennis Mhina ‘John Woka’.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kwa staili yake ya kuimba kama mlevi, Michael Dennis Mhina ‘Joni Woka’ amefariki dunia alfajiri ya leo.

Akiongea kwa simu kaka wa marehemu Omari Milay, amesema walipigiwa simu alfajiri ya leo na kujulishwa kuwa Joni Woka amefariki katika hospitali ya Muhimbili, alipokuwa akipata matibabu ya ajali aliyopata siku ya jana.
Joni Woka alipata ajali ya kugongwa na kitu kizito kwenye paji la uso, alipokuwa garage maeneo ya Sinza akitengeneza gari yake, kwa bahati mbaya mtungi wa gesi ukalipuka na moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani,
Tarifa za awali za madaktari zilisema wanahofia kipande hiko kimefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.
Mipango ya mazishi familia imesema inakutana kujadili na mara itakapokamilika watajulisha watu nini kinaendelea.
Msanii John Woka ambaye alikuwa kwenye kundi la Watukutu Family, alijipatia umaarufu kwa nyimbo zake za Sophia, baby gal na nyinginezo, ambazo aliziimba kwa mtindo wa ulevi.
Kwa yeyote aliyeguswa na angependa kutoa rambi rambi anaweza kuwasiliana na kaka yake kwa namba +255767007005.
Marehemu Michael Denis “John Walker” apumzike kwa Amani.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...