Sunday, February 7, 2016

MIMBA YA WEMA YAMTIA BALAA TUPU!


Staa wa sinema za Bongo, Wema Sepetu.

Hii pia ni habari njema! Kisa mimba, Miss Tanzania 2006 aliye pia staa wa sinema za Bongo, Wema Sepetu amejikuta akiteswa na kitumbo hicho kila kukicha na habari mpya ni yeye kutapika huku wapambe wakisema mbali ya chakula kingine, pia mboga ya majani aina ya matembele ‘tembele’ ilikuwepo, nenda na Ijumaa Wikienda.

Tukio hilo la kiujauzito lilimkuta Wema mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akiwasili kwenye Hoteli ya Slipway iliyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam ambako staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba alikuwa akizindua video yake inayokwenda kwa jina la Lupela. Wema alikuwa na wapambe wake.

MPAMBE AMWAGA SIRI
Mpambe mmoja (jina tunalo) ndiye aliyelipenyezea Wikienda tukio la staa huyo kutapika mbele ya kampani bila kujali mazingira.

“Jamani mimba inamtesa sana madam (Wema). Muda huu tunakuja hapa Slipway wametapika. Yaani ametapika mpaka mboga ya matembele,” alisema mpambe huyo akimwambia paparazi wetu mara baada ya kuingia ndani ya hoteli hiyo.


SASA WEMA ANACHUNGWA
Mbali na wapambe wengine, kuna mwanaume alikuwa sambamba na Wema akihakikisha usalama wake na wa kitumbo huku akiwa karibu kwa lolote.

Mtoboa siri wa Wema alimwambia paparazi wetu kuwa, jamaa huyo ndiye anayemshika mkono Wema kama ataonesha dalili ya kutetereka wakati wa kutembea.

“Huyu mwanaume ndiye mlinzi wa Wema kwa sasa. Kazi yake ni kuangalia kama Wema anaweza kuanguka wakati akitembea au kufanyiwa jambo lolote ambalo linaweza kuumiza makuzi ya mtoto tumboni,” alisema mpambe huyo.

WEMA NA WIKIENDA
Baada ya maelezo hayo, Wikienda lilimfuata Wema na kuzungumza naye mambo makuu mawili. Moja ni kumwomba akubali kupigwa picha akiwa na kitumbo hicho. Pili ni kumuuliza kuhusu kutapika.
Wikienda: “Mambo madam?”
Wema: “Poa, vipi?”

Wikienda: “Poa. Leo naomba nikupige picha.”
Wema: “Mmh! Haya!”
PICHA NA MALALAMIKO
Hata hivyo, wakati Wema akipigwa picha hizo alikuwa akilalama kwamba, hakuwa tayari kupigwa picha akiwa ndani ya gauni la kumbana hivyo kitumbo chake kuonekana.
“Leo ni historia. Sikuwa na mpango wa kupiga picha tumbo langu. Sijui wewe (paparazi wetu) umeninogesha na nini mpaka nimekubali,” alisema Wema.

KUHUSU KUTAPIKA
Wikienda lilimuuliza Wema kuhusu taarifa za kutapika ambapo alikiri:
“Yeah! Nimetapika wakati nakuja hapa hotelini. Ilibidi nishuke kwenye gari (akiendeshwa) ili nitapike vizuri! Kwa kweli tumbo linanitesa sana…huwa natapika.”
Wakati Wema anaulizwa kama alitapika tembele, kuna mtu alimuita hivyo kumuondoa kwenye umakini na paparazi wetu na kuondoka.

ASHINDWA KUTULIA
Baada ya kuachana na paparazi wetu, Wema hakuweza kutulia sehemu moja kwani pitapita yake kila kona huku akiwa amevaa viatu vya mchuchumio (virefu) na kumfanya kila mtu ajue yupo ndani ya nyumba.

MVUTO WAKE
Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida, Wema baada ya kuingia kwenye ukumbi huo, alibadili mazingira ambapo yeye akawa kama ndiyo mwenye shughuli hiyo ya kuzindua video na si Ali Kiba.
Baadhi ya watu walipobaini Wema ameingia, walilipuka kwa nderemo huku kila mtu akitaka kumwona.
Baadhi ya watu walisema: “Jamani kumbe Wema ana mimba kweli?! Si mnaona kitumbo kile! Dah! Aisee! Kweli Mungu mkubwa…mwacheni aitwe Mungu.

“Halafu si alipachikwa kila aina ya jina huyu…wengine walimwita mgumba, wengine tasa, yaani jamani, Wabongo wanaongea sana,” alisikika akisema mmoja wa watu waliohudhuria shughuli hiyo.

WEMA ACHOKA, AONDOKA
Ilipofika saa nane usiku, Wema aliondoka hotelini hapo akiwa na wapambe wake huku akigoma kuongea na paparazi wetu licha ya kupigwa picha nyingine akiwa anasepa.

MAHESABU YA HARAKA
Kwa mujibu wa watu wake wa karibu, mimba ya Wema sasa inagonga mwezi wa nne huku akiwa anaendelea kuhudhuria ‘viwanja’ mbalimbali kwa ajili ya kujirusha jambo ambalo wengi hawakubaliani naye wakisema anajichosha pasipo sababu.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...