Sunday, February 7, 2016

KHAAA... JOKATE AMWANGUA MAMA KIBA!


Jokate akiongea jambo
Mwanamitindo Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’.

 Malovee tena! Siku chache baada mwanamitindo Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ na Mfalme wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, kumwagana, hatimaye habari za chini ya kapeti zimevuja zikidai kwamba Jokate ameamua kumwangukia mama mzazi wa Kiba ili kunusuru penzi hilo na sasa mapenzi yamerudi upya.

Tukio hilo lililonaswa na vyanzo vyetu lilijiri usiku mnene wikiendi iliyopita katika Hoteli ya Slipway iliyopo Oysterbay, Dar mara tu baada ya Kiba kuzindua video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Lupela.
Jokate (kulia), akiwa katika meza ya pamoja na mama yake Ali Kiba (wa kwanza kutoka kushoto).
Kwa mujibu wa watu wa karibu na wawili hao, mara tu baada ya kufika hotelini hapo, Jokate alimfuata mama Kiba na kumsalimia kwa heshima zote kabla ya kuelekea kwa ndugu wengine wa Kiba kisha kurejea kwenye meza ya mzazi huyo.

Mfuatiliaji makini wa tukio hilo aliliambia Ijumaa Wikienda kwamba, Jokate alilazimika kumwangukia mama Kiba ili anusuru hali ya hatari iliyokuwa tayari imeshatokea katika penzi hilo.

“Wewe…(jina la mwandishi wetu) hukujua kinachoendelea, Jokate kamwangukia mama Kiba ndiyo maana umeona ndugu wengine wakiwa karibu kwa muda mrefu ndipo Kiba akaitwa ili akae na Jokate. Si unaona wanapiga stori na kucheka? Sasa hivi mambo safi na mapenzi ni kama zamani,” alisema mmoja wa watu wa karibu wa mastaa hao aliyejua mchongo mzima uliokuwa ukiendelea.

Mbali na maelezo ya mtu huyo, paparazi wetu alibahatika kujionea kwa jicho lake Jokate akiwa ‘klozi’ na mama Kiba na ndugu wengine.Pia mwanahabari wetu aliwashuhudia Jokate na Kiba wakiwa na nyuso za furaha wakifurahia mafanikio ya Video ya Lupela ambayo walisema itafika mbali kutokana na viwango vyake.

Wakati wa kuondoka eneo hilo, Jokate ndiye aliyetangulia kuondoka eneo hilo akiwa ameongozana na marafiki zake na muda kidogo baadaye Kiba alifuata naye akiwa na ndugu zake wengine na kuondoka kwa pamoja.
20SHARES
Jokate katika pozi.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...