Monday, February 15, 2016

LADY JAYDEE APEWA TARAKA YAKE RASMI


Judith Wambura Mbibo ‘Jide
BAADA ya mvutano wa muda mrefu, hatimaye diva wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ amepewa talaka rasmi kwenye Mahakama ya Manzese, Sinza jijini Dar.

Jide alifungua kesi ya madai ya talaka katika mahakama hiyo baada ya kutofautiana na mtangazaji maarufu Bongo, Gardner G. Habash ‘Captain’, aliyekuwa mumewe wa ndoa kabla ya kumwagana takriban miaka miwili iliyopita.

Gardner G. Habash ‘Captain’

Taarifa kutoka kwa chanzo cha kuaminika, wawili hao waliooana mwaka 2005, walitinga katika viunga vya mahakama hiyo Alhamisi iliyopita kisha hukumu ya kesi hiyo kusomwa na talaka rasmi kutolewa kwa Jide na Gardner.

“Nimemuona Jide na Gardner hapa, wamekuja kusikiliza hukumu yao. Taarifa za uhakika ni kwamba tayari mahakama imevunja rasmi ndoa na kila mmoja kapewa hati yake ya talaka na sasa kila mtu yupo huru kuendelea na maisha yake,” kilisema chanzo.

Baada ya taarifa hizo kutua kwenye dawati la gazeti hili, mwanahabari wetu alimtafuta Jide ili aweze kuzungumzia hatua hiyo waliyoifikia lakini simu yake haikuwa hewani kama ilivyokuwa kwa Gardner lakini bahati nzuri mmoja wa ndugu wa mrembo huyo mkongwe wa Bongo Fleva aliyeomba hifadhi ya jina alipatikana na kufunguka:

“Ni kweli tulikuwa mahakamani. Jide ameshapewa talaka yake na kila kitu kimeenda vizuri. Gardner naye kapewa hati yake ya talaka hivyo kuanzia sasa kila mmoja yupo huru kufanya yake.”

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...