Friday, February 19, 2016

HAYA NDIYO MATUKIO KATIKA PICHA MPYA ZA SHILOLE NA BWANA AKE MPYAAAA


Shilole akipata msosi huku mpenzi wake mpya wa sasa Medy Music akimchombeza kwa maneno ya mahaba ili msosi huo uweze kushuka vizuri.
BAADA ya msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kumwagana na aliyekuwa mpenzi wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, hivi karibuni Ijumaa lilinyetishiwa kuwa, amejiweka kwa dogo mmoja aliyefahamika kwa jina la Medy Music ambaye wamekuwa wakipika na kupakua kwenye nyumba ya staa huyo iliyopo Kijitonyama jijini Dar.


Baada ya kunyetishiwa habari hizo, paparazi wetu juzikati jioni alitinga nyumbani kwa Shilole na kufanikiwa kuwakuta wawili hao lakini katika hali ya kushangaza, baada ya kuona kamera wakaanza kufanyiana vituko vya kimahaba.

Shilole na Medy Music wakiperuzi kitu kwenye simu huku furaha ikitawala.

Shilole alionekana kumshikashika Medy huku dogo huyo aliyeonekana kuwa kama kalewa akitoa ushirikiano.Katika meza iliyokuwepo sebuleni kulikuwa na chupa za bia lakini mara kadhaa Shilole alionekana akinywa juisi huku dogo akipiga maji, mazingira yaliyoonekana kuwa Shilole alikuwa akimlewesha kwa makusudi kisha mambo ya ‘kuchi…kuchi’ yachukue nafasi.

Shilole na Medy Music hapa sijui wamegundua jambo gani la kushangaza.

Akizungumzia uhusiano wake na Medy, Shilole alikiri kuwa ndiye mpenzi wake kwa sasa na akawataka wanaodai anambemenda wakidhani ni mtoto wakae kimya.“Huyu ndiye laazizi wangu kwa sasa, ana kila sifa ya kuwa mume wangu na wala siyo mtoto, ni mtu mzima kabisa tofauti na Nuh,” alisema Shilole kisha kuendelea kumdekea jamaa huyo aliyeonekana kafa-kaoza kwa staa huyo.

Wakati Shilole akifanya yake, Nuh naye juzikati alitupia picha kadhaa mtandaoni akiwa kimahaba na demu mkali aliyefahamika kwa jina la Erah Erah anayedaiwa kuwa mpenzi wake.

Mhaba mapya kati ya Shilole na Medy Music.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...