Ostaz Juma Namusoma akiwa katika pozi. |
UKIANZA kutaja majina ya
mameneja mbalimbali wa muziki hapa Bongo, baadhi ya majina makubwa yasiyoisha
miongoni mwao huwezi kulikosa jina la Ostaz Juma Namusoma.
Kwa mujibu wa kinywa
chake mwenyewe Ostaz Juma Namusoma,
juzikati nilipata nafasi ya kumbana na kunieleza kiunagaubaga namna
alivyoweza kujipenyeza hadi kupata jina kupitia muziki wa Bongo.
Ostaz Juma Namusoma akiwa kwenye ubora wake. |
Kwa kinywa
chake aliniambia kwamba, muziki kwake ni sehemu ya maisha ambayo ameishi kwa
kipindi kirefu sana, kwani tangu alipokuwa mdogo alipenda muziki kushinda kitu
chochote, msikie mwenyewe.
OSTAZ JUMA: Mimi ni miongoni mwa vijana wa kipindi
hicho ninayetokea Musoma mkoani Mara.
Nilianza kupenda muziki tangu nasoma
shule ya msingi tena mapema kabisa nikiwa darasa la tatu. Nikiwa shuleni
nilikuwa napenda sana kuimba nyimbo mbalimbali za wasanii wa Kongo hadi nikafi kia hatua ya kununua redio na
kuwarekodi watoto wenzangu wakiimba kisha nazitunza nyimbo walizokuwa
wakishindana kuimba hasa za Boringo za Wazaire.
Ostaz Juma Namusoma. |
Nimefanya hivyo hadi nikawa
nagombezwa na wazazi wangu lakini sikukoma hadi nilipokuwa mtu mzima na kuanza
kujifanyia mambo yangu ambapo wazazi hawakuweza kuniingilia.
Kwa jinsi hii
ndiyo utaweza kugundua kuwa nina kipaji cha kusimamia watu ndiyo maana nimeweza
kuwasaidia wanamuziki wengi tu kwenye dansi ambapo kabla ya kujiingiza katika
Bongo Fleva niliwahi kuwasaidia wanamuziki wa dansi kama Ally Chocky, Super
Nyamwela, Jose Mara, Kalala Junior, Nyoshi ElSaadat, Mwinjuma Muumini na
Mulemule.
Tabia za wanamuziki kiukweli hazipishani sana hivyo ukiona meneja
yeyote analalamika juu ya wanamuziki basi ujue matatizo yao mara kadhaa
yamekuwa hayapishani sana, ila wanaopishana tabia na namna ya kuongoza ni
mameneja tu.
Namna ya kuongoza na kummeneji mtu kunategemeana na uwezo wa
kifedha na akili pia, nasema hivyo kwa sababu muziki wetu umekuwa ukiyumba mara
kadhaa kutokana na baadhi ya mameneja kuwa wasimamizi wabovu na wengine
wanasimamia wakiwa hawana fedha ya kuweza kuwaongoza wasanii.
Meneja ninayeweza
kumpa saluti hapa Bongo ni Saidi Fella kwani ameonesha njia kubwa ya
kuimarisha Muziki wa Dansi na
sasa umeanza kuwa juu kiasi cha watu
kuanza kuupenda tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ulianza kupoteza dira.
ALIANZAJE KUSIMAMIA BONGO FLEVA? OSTAZ JUMA:
Kwenye Bongo Fleva niliingia baada
ya kuanza kumsimamia shemeji yangu aitwaye Abdallah David aliyekuwa akijiita
Fil David, huyu nilijikuta namsimamia baada ya kumuona ana kipaji kizuri na
baadaye nikaanzisha rasmi kampuni yangu ya Mtanashati.
Ostaz Juma katika ubora. |
Mtanashati ilipoanza tu
nikapunguza kuwasaidia wanamuziki wa dansi hivyo nikajikita kwenye Bongo Fleva
ambapo nilianza kumsimamia marehemu Sharo Milionea aliyemleta Kitale, lakini
kabla sijaingia mkataba na Sharo akafariki dunia.
Baada ya kufariki kwa Sharo
Milionea ambaye ndiye msanii naweza kujisifi a katika upande wa Bongo Fleva kwa
kuwa na nidhamu ya hali ya juu sana, nilimchukua PNC, Dogo Janja na Happy Balis
ambao nilifanyanao project kibao kiasi ilifi kia hatua nikawa nakosana hadi na
mke wangu kisa muziki huu.
Ostaz Juma Namusoma |
Nimekuwa nikiwasaidia wasanii hawa kwa muda lakini
nilichoweza kujifunza ni kwamba wasanii wengi hawana adabu kabisa, kwani kuna
siku niliwahi kukosana na mke wangu kwa kushindwa kumpeleka hospitali kisa
kumpeleka Dogo Janja kwenye interview jambo ambalo mke wangu amekuwa
akinikumbusha kila mara nami huwa halitoki kichwani hadi leo.
Fedha niliyowahi
kutumia hadi leo kwa ajili ya Dogo Janja na PNC naweza kujenga hata ghorofa
tatu hapa mjini, lakini kwa kuwa nilikuwa naupenda muziki ndiyo maana leo
utaona inafi kia muda sasa nimeamua kuachana na hawa Bongo Fleva maana hawana
nidhamu hata tone ila ukilinganisha na wanamuziki wa dansi utagundua ni bora
dansi kuliko Bongo Fleva.
Nasema wanamuziki wa dansi ni bora kuliko wa Bongo
Fleva kwa sababu wakati nadili na wanamuziki wa dansi walikuwa wanaonesha
nidhamu ya hali ya juu jambo ambalo wanalifanya hadi sasa.
Ujue nilikuwa
nikiwapatia fedha za kodi za nyumba, mara nyingine kama Christian Bella na
Chocky hawa niliwahi hata kuwalipia studio mara kadhaa kwa ajili ya kurekodi
nyimbo zao binafsi.
Christian Bella yeye aliwahi hadi kunitungia wimbo ambao
unaitwa Ubinadamu ambao hata yeye ukimuuliza leo anaujua na ninao mimi
mwenyewe.
Wasanii wakijua kuwa muziki ni kazi na sehemu ya maisha yao basi
hakuna Bongo Fleva atakuja kushindwa kufanya mambo makubwa kama anavyofanya
Diamond kwani kinachomfanya kuheshimika na kufanikiwa ni nidhamu yake tu.
Ostaz Juma Namusoma |
No comments:
Post a Comment