Wednesday, July 22, 2015

Diamond: Aibu yao!

MSHTUKO! Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefunguka siri nzito kwa mashabiki waliokuwa wakimpigia kampeni katika mitandao mbalimbali ili ashindwe kwenye Tuzo za MTV Africa Music (Mama) 2015, zilizofanyika usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita huko Durban, Afrika Kusini  baada ya kushinda tuzo moja na kudai kuwa ni aibu kwa waliokuwa wakifanya kampeni asishinde.
Diamond-MTVBase-Red-Carpet-03Diamond akiwa katika red carpet ya tuzo hizo.
DIAMOND MTUMBUIZAJI BORA AFRIKA
Diamond alitwaa Tuzo ya Best Live Act (Mtumbuizaji Bora Afrika) ambapo alijikuta akifurahi kupindukia huku akiwakejeli wale waliokuwa wakimpigia kampeni ashindwe kwamba bado ataendelea kuwakalisha vibaya.
WAMEBAKI NA AIBU
“Nina furaha sana kupata tuzo tena, wale waliokuwa wakipiga kampeni kwenye mitandao kwamba nisipigiwe kura naona wamebaki na aibu yaani nimewaumbua, hapa bado ninaongeza nguvu zaidi na nina mpango wa kufanya kazi na mastaa wakubwa wa Marekani, ila ninawashukuru wale walionipigia kura,” alisema Diamond.
JOKATE ALALAMIKA KUDHALILISHWA
Wakati Diamond akisherehekea ushindi huo, mwanadada aliyewahi kuwa mpenzi wake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amelalamika kudhalilishwa mtandaoni na mwanamuziki huyo baada ya kuweka video akiwa anacheza wimbo wa jamaa huyo wa Mdogo Mdogo na kuambatanisha na maneno yaliyosomeka: “Mbona bado. Mtanyooka tu.”
kateJokate.
“Sijapenda na sijawahi kuona mwanaume mswahili kama Diamond, anatafuta kiki za ajabu tu mjini hapa kwani hiyo video ni ya zamani tena nilipigwa nikiwa studio lakini nimeshangazwa sana na kitendo chake cha kuweka kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuambatanisha na maneno ya kunidhalilisha,” alisema Jokate akiwa amepaniki.
Diamond alipata mapokezi ya kifalme  baada ya kutua kwenye Uwanja wa Kimataifa Ndege wa Julius Nyerere, Dar, Jumapili iliyopita ambapo kundi kubwa la watu lilijitokeza kumpokea pamoja na mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye kwa muda mrefu alikuwa mgonjwa lakini alionekana akimfurahia mwanaye uwanjani hapo.
Baada ya kutua Bongo, Diamond alifikishiwa malalamiko ya Jokate kwamba alikuwa amemdhalilisha yeye na wanawake wengine ambapo aliyafungukia:
“Unajua, kwanza nimecheka alafu nimesikitishwa kwa sababu nimeambiwa sijasoma, nimeambiwa kuna posti ameandika (Jokate), amezungumzia vitu vingi…Yeye kacheza kama fan wa nyimbo zangu na mimi nilimposti kama fan wangu.
“Hakuna mahali nilimuandika jina, kwa nini achukulie vibaya?
“Ukiona mtu anajishuku ujue kuna namna nyuma. Mbona mimi naposti watu wengi tu, tena naandika caption zangu za vitukovituko maana yake mimi nina caption za vituko.
“Ni kweli mimi ni mswahili, nimezaliwa Tandale, nimekulia Tandale na Tandale ndiyo kumenifanya leo niwe hapa nilipo…
“Kwa hiyo nina caption zangu za uswahili kwa sababu uswahili ndiyo umenikuza…siziachi kuziandika, huwa naziandika nyingi ..kwa nini ya kwake yeye tu aione tatizo?
kiba6060000000
Ali kiba.
“Kwani kuna ubaya gani mimi kuandika mtanyooka tu kama yeye haimhusu ina maana labda kuna kitu kinamhusu.
“Nimeambiwa pia amezungumza kwamba ndiyo maana wanaogopa kuwasapoti wasanii Watanzania kwa sababu wakiwasapoti wanadhalilishwa, yeye mimi mpaka nimeenda kuchukua tuzo alinisapoti nini?
“Aliposti hata posti moja kusema mpigieni kura Diamond? Sasa hivi anajishaua eti kanisapoti. Amesapoti nini? Eti ametoa hongera, mimi nimeshinda tuzo, eti ooh hongera kwa tuzo by the way, angeposti kuhamasisha watu wapige kura ili ushindi uje nyumbani.

“Lakini kwa chuki alizojazwa zisizo na sababu na roho mbaya aliyowekewa na watu, imemfanya ashindwe hata kuniposti na kutengeneza chuki za chinichini kwa kudhani wakiwapigia kura Wanigeria mimi nitakosa tuzo…mimi nimeshinda, alafu anajifanya kutoa hongera, eti wanasapoti muziki wa Kitanzania, ananisapoti nini, lini amenisapoti au ameona tuzo imekuja ndiyo anajifanya kutoa hongera? Tuacheni unafiki.”
TUJIKUMBUSHE
Awali tuzo hizo zilivyotangazwa watu mbalimbali wakiwemo Timu Ali kiba na wale mahasimu wake walikuwa wakipiga kura za kumpinga Diamond na kumpigia kampeni msanii wa Nigeria, Davido, jambo ambalo mwanamuziki huyo aliwataka kuachana nalo na kuangalia utaifa kwanza.
Miongoni mwa watu ambao hawakuwa wakimsapoti Diamond ni wapenzi wake wa zamani, Wema Sepetu na Jokate ambapo Timu Wema na Timu Diamond zilikuwa zikipambana kila kukicha kutokana na kila upande kumtaka mshindi wao yaani Diamond na wengine wakimpigia kura Davido.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...