Monday, June 22, 2015

WASTARA, ANTI LULU WAPATANA

Safi sana! Mwigizaji Wastara Juma Issa Abeid na Mtangazaji Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’, wamepatana baada ya kuwepo kwa mkwaruzo kati yao kwa muda mrefu, kisa kikielezwa ni mwanaume ambaye ni mwigizaji wa Bongo Movies, Bond Bin Sinan, Ijumaa Wikienda limehusika.
Mwigizaji Wastara Juma Issa Abeid na Mtangazaji Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu wakiwa katika pozi.
Kwa mbwembwe na mapozi tofauti, huku wakiachia sentensi zilizoashiria kila dalili na ishara za ubongo kuchanganyikana na ‘maji ya Ilala’ (pombe) wawili hao walinaswa katikati ya wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar kulikokuwa na harusi ya msanii mwenzao, Haji Adam ‘Baba Haji’.
Awali, mastaa hao walikuwa wameketi viti tofauti huku shamrashamra za sherehe zikiendelea, lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati wa kuondoka, Wastara alimfuata Anti Lulu kwa madai ya kumuaga, ndipo wakasindikizana hadi nje ya ukumbi.
Kabla ya Wastara kuingia kwenye gari lake, wawili hao walikumbatiana kwa furaha huku wakiangua vicheko vya ‘kushabikia ushindi’, jambo lililozua miguno na viulizo miongoni mwa wasanii wenzao.
Ndani ya dakika sifuri, Ijumaa Wikienda lililokuwa limepenyeza ‘kijumbe’ wake kwenye pati hiyo, liliwafotoa picha kisha kuwahoji kulikoni wawe na furaha ya namna hiyo licha ya kuwepo kwa tetesi zikiwahusisha na bifu?
“Sisi ni wanawake, hatuwezi kununiana,” alisema Wastara na Anti Lulu kushadadia.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...