Tuesday, June 9, 2015

MAI AMCHOKONOA LINAH

KATIKA kinachoonekana kama kumchokonoa nyota wa muziki Estalina Sanga ‘Linah’, mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’ ameunga mkono kitendo cha Wema Sepetu kumchukua mpenzi wa Mbongo Fleva huyo Nangari Kombo.
 
Mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’.
Mai aliweka picha ya Wema akiwa na Kombo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumpongeza kwa kumpata ingawa watu mbalimbali walimponda mtangazaji huyo kwa maneno makali wakimlaumu kwa kufurahia mwenzake kuporwa bwana.
Gazeti hili lilipomtafuta na kumuuliza kuhusu kisanga hicho, Mai alisema; “Jamani Wema naye ni binadamu na ana haki ya kuwa na mpenzi, mimi sijui hizo habari kwamba amemchukua mwanaume wa Linah, nilimpongeza kwa sababu ni mdogo wangu, kwa kumpata mpenzi kwani mjini mwanamke ukionekana kila siku uko peke yako wanakufikiria vibaya na kuongea maneno mengi ya ajabu.”

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...