Monday, May 25, 2015

VINARA WA ‘KUUZA MECHI’ MAMA TOFAUTI!


Watu wengi ambao wamejikuta wakipata watoto wengi kwa wanawake tofauti, wanatafsiriwa tofauti kwenye jamii. Wengine wanaonekana siyo makini katika suala la kujilinda kwa maana ya matumizi ya kinga kwa lugha ya watoto wa mjini hutumia msemo wa ‘kuuza mechi’ bila kujali umuhimu wa afya zao.
Staa wa Bongo fleva, Ali Kiba.
Kama hujaelewa, Kuuza mechi ni kushiriki tendo la ndoa bila kinga. Wakati mwingine hutokea kwa bahati mbaya lakini kama itatokea zaidi ya mara moja, lazima watu watakuwa na mtazamo tofauti na wewe, inaonesha ni jinsi gani ni kinara kwenye suala hilo la kuuza mechi.
Uchunguzi unaonesha kuwa kwenye ulimwengu wa mastaa Bongo, kuna wasanii lukuki ambao kwa namna moja au nyingine wameshiriki katika ishu hiyo na matokeo yake ni kuwa na watoto waliozaliwa nje ya ndoa.
Makala haya yanakuletea listi ya vidume mastaa wa Bongo ambao wana watoto waliozaa na wanawake tofauti;

 
Msanii wa Bongo Fleva, Dully Sykes.
ABDUL SYKES ‘DULLY’ (watoto watatu)
Huyu ni legendary wa Bongo Fleva ambaye hivi karibuni alifikisha miaka 15 katika muziki anaoufanya. Ana watoto watatu ambao anakiri kuzaa na wanawake tofauti ingawa majina ya mama zao huwa ni siri yake.


ALI SALEH KIBA (watoto watatu)
Kiba ni staa mkongwe mwenye mashabiki wengi anayekimbiza na mzigo mpya wa Chekecha Cheketua. Jamaa huyu anaingia katika orodha ya wauza mechi kwa kuwa anakiri kuwa na watoto watatu aliozaa na wanawake tofauti.
Q-Chillah akifikiria jambo wakati akihojiwa na Global TV Online.
ABOUBAKAR KATWILA ‘Q CHILLAH’ (watoto watatu)
Chillah kama ilivyo Dully naye ni legendary wa Bongo Fleva. Jamaa anakiri kuwa na watoto watatu, akiwa amewapata kwa wanawake tofauti ambao siyo mastaa kama alivyo yeye.

KHALEED MOHAMED ‘TID MNYAMA’ (watoto wawili)
Huyu ni mkali wa ngoma kibao kama Zeze, Nyota Yangu, Siku Kama Hizi, Kiuno na nyingine kibao ambazo ziliwahi kuwa nyimbo za taifa. Jamaa ana watoto wawili akiwa amezaa na wanawake tofauti. Mmoja alikuwa maarufu aliyejulikana kwa jina moja la Kinana.
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Khaleed Mohamed 'TID'.
EMMANUEL ELIBARIKI ‘NAY WA MITEGO’ (watoto watatu)
Jamaa anatikisa kwenye Bongo Fleva kwa sasa. Nay anaingia kwenye orodha hii akiwa na watoto watatu, mmoja alizaa na dada wa Kihindi (jina halifahamiki), akazaa na msanii wa Bongo Movies, Skyner Ally na mtoto wa mjini, Siwema Edson.

MACK SEKIMANGA ‘MAKAMUA’ (watoto wawili)
Jamaa ni mmoja wa wakali wa RnB Bongo aliyewahi kutamba na ngoma kama Tell Me Why na nyinginezo. Hakosi kwenye orodha hii kwa sababu ana watoto wawili ambapo kila mmoja ana mama yake.

KULWA KIKUMBA ‘DUDE’ (watoto saba)
Jamaa ‘bana’ ni tishio na  ndiye anaongoza kwa kuwa na watoto wengi kwa wasanii wa Bongo. Dude  ana watoto saba kwa wanawake wanne tofauti. Siku zote amekuwa muwazi kuhusu suala hilo.
(Makala: Gabriel Ng’osha/GPL)

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...