Monday, May 11, 2015

PART II YA SAKATA LA ADEBAYOR NA FAMILIA YAKE; AMCHANA MDOGO WAKE AITWAYE ROTIMI, KUTOKA PART III HIVI KARIBUNI


Emmanuel Adebayor akiwa na mdogo wake Rotimi Adebayor.
KAMA alivyoahidi, staa wa Klabu ya Tottenham ya England ambaye ni raia wa Togo, Emmanuel Adebayor jana ameachia sehemu ya pili inayohusu sakata lake na familia yake. Katika sehemu hii, Adebayor amemuelezea kaka yake aitwaye Rotimi.

Na hivi ndivyo alivyomwaga ubuyu kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo ameahidi pia kutoa sehemu nyingine ya tatu hivi karibuni:
Hii ni sehemu nyingine ya stori ambayo nimeiweka kwa muda mrefu ila leo nahisi ni muda muafaka kuiachia hadharani.
Ninapoweka stori hizi na kuwashirikisha, ni kwa sababu naamini kila stori inakuja na funzo. Na funzo hilo ni kwa kila mmoja wetu anayesoma stori hizi.
Stori hii inamuhusu kaka ambaye amekuwa akiongea kuwa mimi siisaidii familia yetu.
Jina lake ni Rotimi Adebayor. Akiwa na umri wa miaka 13, alifanya kitu kibaya sana.
Ni mimi na yeye pekee ndiyo tunajua alichokifanya. Kutokana na kitu hicho, wazazi wetu waliamua kumpeleka kwenye kijiji kimoja cha mbali kutoka kwenye mji mkubwa.

Nilipoanza kufanikiwa katika soka na kwenda nchini Togo kwa ajili ya likizo; Mmoja wa marafiki wa mama yangu alikuja kututembelea akitokea kijijini.
Alivyotueleza jinsi Rotimi alivyokuwa akitaabika huko kijijini, kwa haraka niliwaambia wamrudishe tena mjjini. Mara tu alipofika mjini,nilihakikisha nampeleka shule. Kwangu hilo ni suala la kawaida.
Mwaka 2002, nilikwenda kushiriki Fainali za AFCON nchini Mali na kupata fursa muhimu ya kubadilishana jezi na Marc-Vivien Foé. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema.
Niliporudi Togo, niliweka jezi hiyo katika eneo salama. Kaka yangu huyo alitumia mbinu zake na kuiba jezi hiyo na kuiuza.

Nilipohama kutoka Metz kwenda Monaco, tulifanikiwa kufika katika hatua ya juu kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Balani Ulaya na tulicheza na Klabu ya Real Madrid.
Siku hiyo ilikuwa ni mojawapo ya siku nzuri na muhimu katika maisha yangu maana nilipata bahati ya kupata jezi iliyokuwa imesainiwa na lejendari wa soka Zinedine Zidane.
Nilipoipeleka jezi hiyo Togo, kaka yangu yuleyule aliiba jezi hiyo na kuiuza.
Nilipokuwa Metz, nilikuwa nikilipwa €15,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 33 za Kitanzania kwa mwezi.
Nilitaka kumpatia mama yangu mzazi kitu cha kipekee kumshukuru kwa yote aliyonitendea, Nilitaka kumfanya awe na furaha.
Hivyo niliamua kuchukua fedha ya mishahara yangu ya miezi mitatu na kumnunulia mkufu wa dhahabu wenye dhamani ya takribani €45,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 100 za Kitanzania.
Rotimi na marafiki zake akina Akim(@Yam Freedom) na Tao (@Sao Tao Oyawole) walifanya mpango na kuiba mkufu huo wa gharama na kuuza kwa €800 sawa na zaidi ya shilingi milioni 1.7 za Kitanzania.
Mimi na mama tulipogundua, mama aliniambia nisijali maana huyo ni mdogo wangu.
Mbali na hayo yote yalyotokea, napenda kuchukua fursa hii kuwatakia heri akina mama wote katika siku yao ya leo ya ‘Mother’s Day!’
Ndani ya nyumba yangu, nina chumba maalum ambapo nahifadhi baadhi ya vitu vyangu pale ninaposafiri kwenda Ulaya.
Ni mimi pekee mwenye ufunguo wa nyumba hiyo ila kaka yangu huyo aliweza kutengeneza ufunguo wenye uwezo wa kufungua kila chumba cha nyumba hiyo.
Mara kwa mara alikuwa akiingia na kuiba vinywaji na vitu vingine kutoka ndani ya nyumba huyo.
Mbali na mambo yote haya tuliendelea kusema kuwa “damu ni nzito kuliko maji” na maisha yalizidi kusonga.
Baada ya hapo niliamua kumpeleka nilipoanzia safari yangu ya soka huko nchini Ufaransa.
Nilimpeleka katika kituo kimoja kikubwa cha soka Ufaransa. Utakuwa tayari unajua stori hii itakapoishia.
Aliiba simu za mkononi kutoka kwa wachezaji wenzake wengi na alifukuzwa katika kituo hicho cha soka.
Baada ya mimi kutoa stori ya kwanza kuhusu yeye, aliamua kunipigia simu na kuniambia kuwa hakuiba idadi hiyo kubwa ya simu 21. Alilalamika kuwa idadi ya simu ilikuwa ndogo kuliko niliyotaja.
Bado..hilo si kosa? Pia aliongeza kuwa inabidi nifurahi kwa kuwa alikuwa akiiba vinywaji na vitu vingine kutoka kwenye nyumba nilipokuwa nimehifadhi vitu vyangu. Nilipomuuliza kwa nini, alinijibu kuwa: “Kwa sababu mimi ni kaka yako”
Jacques Songo’o raia wa Cameroon ambaye kwa sasa amestaafu soka naye alikuwa na kijana katika kituo hicho cha soka Ufaransa na alikuwa rafiki wa karibu wa Rotimi.
Ngoja niongeze kuwa Songo’o alikuwa mmoja wa watu waliosaidia kukuza soka langu na mara nyingi alinipa ushauri mzuri.
Nilikuwa Togo wakati wa mapumziko yangu ambapo Songo’o alinipigia simu; aliongea kwa hasira. Alinieleza jinsi mdogo wangu alivyomuibia kijana wake PlayStation Portable (PSP) yake. Nilipomuuliza mdogo wangu kwa nini alifanya hivyo, alijitetea kuwa kijana huyo alisahau PSP hiyo kwenye begi lake.
Unawezaje kusahau kifaa cha mtu katika begi lako na kusafiri kutoka Ufaransa mpaka Togo? Tangu siku hiyo, ukaribu wangu na Songo’o ukapotea na kwa sasa amekuwa mbali na mimi pamoja na familia yangu.
Nilikuwa bado Monaco nilipoamua kukusanya viatu vyote vya wachezaji wenzangu ili nivipeleke
kwa ajili ya watu wa Afika.
Nilikuwa na begi kubwa lililojaa viatu. Nililisafirisha begi hilo mpaka Togo. Siku chache baada ya kuamua kuwa nitatoa viatu hivyo kwa watu wahitaji, niligundua kuwa begi hilo lililojaa viatu halipo. Baadaye, nilikuja kugundua kuwa kaka yangu (Rotimi) ndiye aliyeiba begi hilo na alikwenda kuuza viatu hivyo huko Hedzranawoé (soko maarufu la umma nchini Togo).
Siku moja, mama yangu alinipigia simu alfajiri nikiwa bado kitandani. Aliniambia kuwa Rotimi amepata Visa ya kwenda Dubai, hivyo anaweza kucheza soka huko.
Ilibidi aondoke siku hiyo akiwa na rafiki yake Kodjovi (@Denilson de Souza) ambaye naye alikuwa anakwenda kwa ajili ya tukio kama hilo.
Ilibidi waondoke siku hiyo au Visa ingesitishwa. Nilimuomba mmoja wa marafiki zangu wa wakati huo (@Agui Mozino) kwenda kunitafutia tiketi kwa ajili ya mdogo wangu pamoja na rafiki yake. Hatukufanikiwa kupata tiketi za ‘economy class’ kwa siku hiyo, hivyo niliamua kuwakatia wote tiketi za ‘first class’.
Pamoja na hayo, ilikuwa ni fursa kwake kutengeneza maisha yake ya soka huko Dubai.
Siku nne baadaye, Rotimi alirejea nyumbani. Alieleza jinsi maisha ya Dubai yalivyomshinda. Alieleza kuwa hakuwa huru kufanya alichotaka kukifanya kwa sababu sehemu hiyo ni mahsusi kwa ajili ya Waislamu. Kwamba hasingeweza kunywa pombe, kwenda kwenye pati kama alivyotaka au kubusu wasichana waziwazi.
Sehemu ya tatu itakujia hivi karibuni na itakuwa ikimzungumzia mwanaume anayejiita Baba wa Familia @Kola Adebayor A.K.A Simba wa Yuda.
Alimalizia staa huyo kutoka Togo.
JE, KWA MAONI YAKO UNAONA NI SAHIHI KWA ADEBAYOR KUENDELEA KUANIKA MAMBO YAO YA KIFAMILIA HADHARANI? NI NENO GANI UNALO LA KUMSHAURI STAA HUYO?

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...