Wednesday, May 20, 2015

Mr T touch: Studio (Free nation) ni yangu, si ya Ney wa mitego. Created by TimesFM Radio on Wed, 05/20/201Mtayarishaji wa muziki grade one Bongo kutoka Free nation records Mr T touch, amefunguka kuwa studio hiyo mmiliki ni yeye na si ya mwanamuziki Ney wa Mitego kama wengi wanavyodhani.
Akipiga story kupitia kipindi cha “The jump off” cha Times fm, Thabeet “ Mr T” amesema amesikia sana mtaani hata kwenye vyombo vya habari kwamba Ney ndiye mwenye Free Nation lakini si kweli bali alitoa msaada.
“Jamaa katoa fadhira producer wake kwa kufungua free nation, ila mimi ndio namiliki alichokifanya ni amekumbuka vikubwa nilivyo mfanyia, afu ukicheki zamani alikua hanilipi so ye kapiga show akaona anapaswa kunisaidia nitimize ndoto zangu” alisema T
Kwenye line nyingine MR T ametoa deal la maradhi(sehemu ya kulala), kwa wasanii wa mikoani wanaokwenda kurekodi ngoma “Free nation”.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...