Na Musa Mateja
ILIANZA kama utani lakini
siku zilivyosonga ndivyo uhusiano wao ulivyowekwa wazi, hao ni watu wawili
waliowahi kuwa maadui wakubwa miaka kadhaa nyuma.
Hapo nawazungumzia staa wa
filamu Shamsa Ford na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’
ambao kwa sasa wamezama kwenye mahaba niue.
Awali, wahusika wote
walitumia nguvu kubwa kukanusha juu ya uhusiano wao lakini inatajwa kuwa mahaba
yao ndiyo gumzo kuliko ya wengine wote katika Bongo Muvi na yanashika nafasi ya
pili katika Bongo Fleva nyuma ya Diamond na Zari kwa sasa.
Awali, uadui wao ulitokana na
Nay kuwaponda wasanii wa kike wa Bongo Muvi na kudai wengi wao hawana lolote na
kazi yao ni kujiuza, Shamsa alikuwa mmoja wa waliopokea kwa hasira kali na
kumbwatukia Nay lakini ule usemi kuwa ‘wagombano ndiyo wapatanao’, ulikuwa
unawahusu.
Walipoulizwa juu ya mahabati
yao baada ya picha kuvunja mitandaoni wakipeana ‘mabusu’ motomoto hivi
karibuni, walisema wana ‘project’ maalum ya filamu.
Sasa inavyoonekana filamu yao
imekuwa ya ukweli badala ya zile za kuigiza. Pichani ni jinsi mahaba nigaragaze
yalivyotawala katika maisha ya wawili hao.
ambacho kitamtengenezea zaidi kipato.
No comments:
Post a Comment