Tuesday, May 12, 2015

WASANII‭ ‬BONGO‭ ‬MOVIES NI NANI ALIYEWAROGA‭?

 
KWENU wasanii wa Bongo Movies‭. ‬Bila shaka mko poa na mnaendelea na mishemishe zenu za mjini kama kawaida‭. ‬Kutokana na ubize wa kazi zenu na zangu‭, ‬leo nimeona bora niwakumbuke kwa barua‭.‬
Mkitaka kujua hali yangu‭, ‬mimi ni mzima wa afya namshukuru Mungu naendelea na majukumu yangu kama kawaida ambapo moja ya majukumu hayo‭, ‬ni hili la kuwaandikia barua kuwakumbusha pale ninapoona hamuendi sawa au kuwapongeza mnapofanya vizuri‭.‬
Dhumuni la barua hii ni kutaka kuwauliza ni nani amewaroga‭? ‬Imefika hatua nimeona niwaulize swali hilo kutokana na mustakabali mzima wa mvuto wa sanaa yenu uliopo kwa sasa‭.‬Kutokana na kazi yangu‭, ‬mbali ya kufanya kwa ukaribu na makundi mengine ya kijamii‭, ‬nimefanya na nyinyi kwa muda mrefu kidogo‭, ‬najua baadhi yenu mtakuwa ni mashahidi wa hili‭.‬

Pointi yangu hapa ni hii‭. ‬Kuna wakati nyinyi wasanii wa filamu mlikuwa juu sana kimauzo‭, ‬umaarufu na hata mafanikio kwa jumla‭. ‬Mlikuwa ndiyo mnaozungumzwa mitaani na kila rika‭. ‬Si watoto‭, ‬mama na hata baba zao‭. ‬Sinema zilikuwa‭ ‬‮!‬٪zinakamata‮!&‬‭ ‬watu kwelikweli‭.‬
Si mnakumbuka kipindi kile mlivyokuwa mnaonekana nyinyi tu hata katika muziki wa bendi‭, ‬watakuwepo mastaa wengi ukumbini lakini‭ ‬utasikia majina ya wasanii wa Bongo Movies‭ ‬‮!‬٪yakirushwa‮!&‬‭ ‬ukumbini‭. ‬Mitaani kwenye‭ ‬‮!‬٪vibanda-umiza‮!&‬‭ ‬ilikuwa kila mmoja anazungumzia mastaa wa sinema pengine kuliko mastaa wa muziki‭, ‬wanasiasa na‭ ‬hata wanamichezo‭. ‬Lakini kwa takriban miaka mitatu iliyopita ufalme wenu umepokwa na Bongo Fleva‭.‬
Sasa hivi watoto wanamjua Diamond‭, ‬Ali Kiba na wengineo lakini si nyinyi tena‭. ‬Wanafuatilia kazi zao‭, ‬wanafuatilia habari zao‭. ‬Wanataka kujua wanafanya nini katika maisha yao ya sanaa kila siku‭. ‬Mafanikio ya wasanii wa muziki yanaonekana dhahiri‭. ‬Mashabiki‭ ‬wanaona wanavyovuka mipaka‭, ‬wanaona wanafanya shoo na kutengeneza mamilioni katika nchi za watu‭.‬
Upande wenu kimya kimetawala‭. ‬Si kwamba hamtoi muvi‭, ‬la hasha‭. ‬Mnatoa lakini mvuto umepungua‭. ‬Watu hawazifuatilii sababu mvuto wenu umeshuka‭. ‬Sinema mnazitoa‭, ‬Wabongo hawaoni zile mishemishe za nyinyi kutangaza kazi mpya‭, ‬kufanya matamasha makubwa ya sinema‭, ‬kuvuka mipaka ya Tanzania hata kwa kufanya ziara katika nchi za jirani kama ilivyokuwa kipindi kile cha kina Vincent Kigosi‭ ‬‮!‬٪Ray‮!&‬‭, ‬Steven Kanumba‭ (‬marehemu‭) ‬na wengineo‭.‬
Ndugu zangu mbona mliweza kipindi kile halafu sasa mshindwe‭? ‬Hata kama mnashindwa kwenda kwa pamoja jitihada binafsi zinahitajika‭. ‬Pigeni kazi za‭ ‬‮!‬٪individual‭,‬‮!&‬‭ ‬vukeni mipaka kwa nguvu zenu tuone mnatoboa‭.‬
Msikae mbali na vyombo vya habari‭, ‬mnajiharibia wenyewe bila kujijua‭. ‬Fanyeni kazi‭, ‬zifikisheni kwenye media kazi zenu zitangazwe na si kuweka chuki na waandishi halafu baadaye mnakuja kulaumu kwamba mnatengwa‭.‬
Najua mnaweza‭, ‬naamini mnaweza kuamka na kufanya mambo makubwa ya kushangaza‭. ‬Fanyeni kweli na sisi tutawapa sapoti‭! ‬Kutakapokucha

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...