Tuesday, May 12, 2015

BARCELONA YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA


Neymar, Luis Suarez na Lionel Messi wakishangilia bao.
BARCELONA imefanikiwa kufuzu hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kufungwa mabao 3-2 na Bayern Munich usiku huu jijini Munich nchini Ujerumani.

Thomas Muller akiifungia Bayern bao la tatu usiku huu.
Barcelona imefuzu kwa jumla ya mabao 5-3 baada ya kupata ushindi wa 3-0 katika mechi yao ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Bayern huko Hispania.

Gerard Pique akikwaana na starika wa Bayern, Robert Lewandowski, aliyekuwa amevaa mask baada ya kuvunjika pua yake.
Mabao yote mawili ya Barcelona yamefungwa na Neymar 15, 29 huku ya Bayern yakifungwa na Benatia 7, Lewandowski 59, Muller 74.
Kwa matokeo hayo Barcelona wanasubiri kucheza fainali Juni 6, mwaka huu na mshindi wa mechi kati ya Real Madrid na Juventus.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...