Wednesday, April 22, 2015

MMOJA WA VIJANA WALIONASWA KWA UJAMBAZI DAR ALIMVISHA PETE MCHUMBA WAKE HIVI KARIBUNI

Mmoja wa vijana walionaswa kwa ujambazi jana akiwa na msichana anayedaiwa kumvisha pete hivi karibuni.
Vijana wanne walionaswa katika tukio la ujambazi jana. Wa pili kulia ndiye anayedaiwa kumvisha pete mchumba wake hivi karibuni.
Vijana hao wakiwa chini ya ulinzi baada ya kutiwa nguvuni.
MMOJA wa vijana wanne walionaswa jana katika tukio la ujambazi eneo la Mataa ya Red Cross katikati ya Jiji la Dar es Salaam, hivi karibuni anadaiwa kumvisha pete msichana mmoja ambaye ni mchumba wake.
Vijana hao walitiwa nguvuni na Jeshi la Polisi jana baada ya kuvamia na kumpora fedha raia mmoja wa kigeni eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Baada ya kufanya tukio hilo, vijana hao walifanikiwa kukimbia na gari walilokuwa nalo ila kulikuwa na msamaria mwema mmoja aliyeona tukio hilo ambaye aliweza kufukuzana nao akiwa na gari yake na kufanikiwa kuwapita mbele na kuwazuia na hivyo kushindwa kupita na gari walilokuwa nalo ndipo askari kufika na kuwaweka chini ya ulinzi.
Vijana hao wanne ambao ni watanashati na ni vigumu kudhani kuwa wanaweza kujihusisha na vitendo vya ujambazi, baada ya kukamatwa na polisi walikutwa na bunduki mbili.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...