HABARI ikufikie kuwa muuza nyago wa video za wasanii wa Bongo Fleva
(video queen), Agness Gerald ‘Masogange’ anadaiwa kutimuliwa nchini
Afrika Kusini ‘Sauzi’ na sasa amekuwa akionekana Bongo akirandaranda
mitaani.
TUJIUNGE JOHANNESBURG
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho
Masogange ni rafiki yake aliyeko maeneo ya Midland jijini Johannesburg,
Sauzi, staa huyo alitimuliwa na mwenye nyumba baada ya kodi ya pango
kwisha na kutakiwa kulipa jambo ambalo lilimshinda.
Ilisemekana kwamba mwanaume aliyekuwa akimpa jeuri aliyetajwa kwa
jina maarufu la Said 2010 ambaye ni mfanyabiashara, Mbongo aishie jijini
humo alimtosa hivyo bidada akarejea Bongo kinyemela.
KUMBE CHANZO NI TUNDA
Habari nzito zilidai kwamba chanzo cha
jamaa huyo ‘kumfungia vioo’ Masogange ni baada ya kunasa kwenye penzi la
muuza nyago mwingine wa video za wasanii wa Kibongo aliyetajwa kwa jina
maarufu la Tunda.
Ilidaiwa kwamba zile mbwembwe za Masogange za kujitundika mitandaoni
zilifika mwisho baada ya Said kuhamia kwa Tunda, mtoto mweupe mwenye
sura ya mvuto ambaye anaonekana kwenye video za nyimbo za akina Matonya,
TID ‘Mnyama’, Christian Bella na wengine wengi.Ilizidi kunyetishwa
kwamba, awali, Tunda alikuwa Bongo lakini jamaa huyo alimtumia tiketi ya
ndege na sasa anatanua naye Bondeni kwa Madiba.
UGOMVI
Ubuyu uliendelea kumwagwa kwamba, hivi karibuni Masogange
na Tunda waliingia kwenye ugomvi mkubwa huku wakitukanana mitandaoni
bila kuanika sababu ya bifu lao.
“Kama ulikuwa unamfuatilia Masogange wiki mbili hivi zilizopita,
utagundua kuna mtu alikuwa anagombana naye. Si mwingine ni huyo Tunda
ambaye amemdatisha jamaa hadi akasahau kama kuna Masogange.
“Wewe
fikiria, Masogange siyo mtu wa kutua Bongo kimyakimya bila kutupia picha
kwenye Instagram ili kuwarusha roho wenzake. Siyo kwamba hawezi, sasa
hivi yupo juu ya mawe ndiyo maana anajificha,” kilisema chanzo hicho.
SUALA LA URAIA
Chanzo hicho kilipotonywa kuwa mwaka jana
Masogange alitamba kuukwaa uraia wa Sauzi na kuukana wa Bongo
kilisema:“Mimi nimeishi hapa South Africa (Sauzi) zaidi ya miaka mitano.
Nilishaomba uraia miaka kibao sijapata hadi leo, huyo Masogange ni nani
wampe uraia kwa siku mbili? Hizo fiksi tu. Kama aliomba sawa lakini
hawezi kupewa uraia kirahisirahisi. Kuna process (taratibu) ndefu hadi
mtu apate uraia.”
MASOGANGE ATAKWENDA TENA SAUZI?
Chanzo hicho kilizidi kudadavua
kuwa siyo kwamba Masogange hatakwenda tena Sauzi kwa sababu ana watu na
marafiki kibao nchini humo lakini kwa sasa hana maskani ya kufikia baada
ya kutimuliwa.“Anaweza kwenda any time (muda wowote) lakini mpaka awe
na uhakika na pa kufikia,” kiliongeza chanzo hicho.
Baada ya kujazwa habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Masogange,
alipopatikana alisomewa kila kitu ‘eituzedi’ ambapo aliomba chondechonde
isiandikwe kwamba ametimuliwa bali yupo Bongo kwa ajili ya mapumziko.
“Jamani si kweli, waambie wahariri nipo huku (Bongo) kwa ajili ya mapumziko tu,” alisema Masogange kwa kifupi.
TUJIKUMBUSHE
Mwaka juzi Masogange alikamatwa Sauzi kwa msala wa
madawa ya kulevya ambapo alihukumiwa kisha akalipa faini na kurejea
Bongo kabla ya baadaye kutangaza kupata uraia nchini humo.
No comments:
Post a Comment