Thursday, April 9, 2015

ETI MAYA, JOHARI WANA GUNDU


Msanii wa kitambo katika tasnia ya filamu Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’, amefunguka kuwa anahisi yeye na mwigizaji mwenzake ambaye ni mkongwe, Blandina Chagula ‘Johari’ wana gundu kwani wasanii wenzao wengi wana watoto na wengine ni wajawazito lakini wao wapowapo tu.
Mwigizaji mkongwe Blandina Chagula ‘Johari’.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Maya alisema kuwa kuna wakati anakaa na kufikiria sana hatma yao na kuona kwamba kama imeshindikana kuolewa basi wapate hata watoto angalau nao wajidai kama wenzao.
Msanii wa kitambo katika tasnia ya filamu Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’.
“Mimi na Johari ni wasanii wakongwe sasa sijui ni gundu ama nini, kama hatupo kwenye listi ya wale wa kuolewa basi tupate hata mtoto mmojammoja maana mimi naona tunazidi kuzeeka kabisa kila siku inayoenda kwa Mungu,” alisema Maya.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...