Thursday, April 9, 2015

KADJA: KWA MAISHA HAYA MUME WA NINI?

Musa Mateja
STAA kutoka nyumba ya kukuza vipaji Tanzania ‘THT’, Khadija Maige ‘Kadja Nito’,  hatimaye ameamua kufunguka na kusema kuwa, kwa maisha yake ya sasa ya kimuziki haoni kama kuna umuhimu wa kufikiria masuala ya kuolewa.
Staa kutoka nyumba ya kukuza vipaji Tanzania ‘THT’, Khadija Maige ‘Kadja Nito’.
Akizungumza na paparazi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita Kadja alisema kuwa, muziki sasa ndiyo kila kitu kwake hivyo hawezi kumpa nafasi mwanaume au kuzungumzia suala la ndoa hivi sasa.
“Naweza kuishi maisha yangu bila mwanaume, napata mshiko, nawasaidia ndugu zangu na mimi najimudu, mume wa nini maisha haya? Sasa ni muziki na mimi, mimi na muziki, mapenzi yasubiri,” alisema Kadja.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...