Thursday, March 26, 2015

WANAKWAYA: JOKATE ANATUTIA AIBU

Musa Mateja
TUMUOMBEE! Afya ya mama mzazi wa msanii nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz, Sanura Kassim ‘Sandra’ bado si shwari juzikati hali yake ilibadilika ghafla na kuilazimu familia yake kumkimbiza katika Hospitali ya TMJ iliyoko Mikocheni jijini Dar ambako amepewa kitanda, Ijumaa limetonywa.
Msanii nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz akiwa na mamaake.
Chanzo cha uhakika kililieleza gazeti hili kuwa mama Diamond ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi yenye kuashiria kupooza, juzikati alizidiwa na kusababisha ndugu zake wampeleke hospitali.
“Mamake Diamond ana wiki sasa hospitalini, lakini mwenyewe Diamond hataki watu wajue, anakwenda kwa kujificha, wakati mwingine hadi saa saba usiku, sijui anaficha nini wakati suala lipo wazi tu, nadhani tukeshe tukimuombea ili hali yake iweze kurudi kama zamani,” kilisema chanzo chetu.
Gazeti hili lilifunga safari hadi hospitalini hapo ili kujiridhisha juu ya habari hizo, lakini mhudumu mmoja aliyeulizwa juu ya uwepo wa mama huyo, alikubali kuwa ni kweli amelazwa hapo, lakini lisingeweza kuruhusiwa kumuona bila ruhusa ya Diamond au wanafamilia.
Akipozi na mamaake.
Diamond alipotafutwa kuzungumzia afya ya mama yake aligoma kusema lolote zaidi ya kuomba aachwe kwani wanao uwezo wa kuzungumzia mambo mengine bila kugusia kuhusu mzazi wake.“Naomba unipe muda maana nina matatizo sana, hata kuzungumzia ishu hiyo nadhani hakuna haja,” alisema Diamond.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...