Friday, March 27, 2015

HUKUMU DNA MTOTO WA NAY APRILI 8 MWAKA HUU

LILE sakata la mtoto si wa Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa mujibu wa madai yaliyotolewa na mzazi mwenzake, Siwema limeingia hatua nyingine baada ya ofisi ya mkemia mkuu wa serikali kusema majibu kamili ya kipimo cha vinasaba ‘DNA’ yatatolewa Aprili 8, mwaka huu.
Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa na mzazi mwenzake Siwema pamoja na mtoto wao.
Akizungumza na Risasi Jumamosi juzi jijini Dar, Nay alisema kila kitu kimekwenda sawa, hivyo anachosubiri ni hayo majibu ili ajue moja kwamba mtoto huyo mwenye miezi mitatu  ni wa nani kati yake yeye na mwanaume aliyetajwa na Siwema mwenyewe.
“Ndiyo natoka sasa kwenye ofisi ya mkemia. Hukumu ya DNA ile ni baada ya wiki mbili kuanzia leo (juzi Alhamisi). Lakini we acha tu. Mh! Nimeshafanya kila kitu, ni wao tu,” alisema Nay.
Aliongeza: “Ila mimi nashangaa. Yule mkemia aliyenipima, kaniambia, ‘Nay hukuwa na haja ya kupima DNA, mbona kwa uzoefu wetu hapa ukimwangalia mtoto anaonekana ni wako, ila kwa sababu umeamua kupima mwenyewe sawa.
‘Nay wa Mitego’ akiwa na Siwema.
“Nimeamua hivi ili mtoto aje kuwa na amani ukubwani, maana ujue atakapokua atakumbana na madai ya mama yake kwenye mitandao, sasa ni bora aje ajue ufumbuzi ulipatikanaje. Kama baba ni mimi au yule mzee anayemsema Siwema atajua.”
Risasi Jumamosi: “Hivi Nay, ikithibitika mtoto si wako utafanya nini?”
Nay: “Namrudisha kwa mama yake maana mimi nitakuwa baba haramu.”
Nay alisema siku ya kupima damu, alikwenda yeye na mtoto huyo ambapo walitumia dakika saba kutolewa damu kwa wote wawili. Bado mtoto huyo anaishi naye nyumbani kwake, Kimara, Dar.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...