Saturday, March 14, 2015

SHOO YA USIKU WA ISHI KISTAA YAFANA DAR

Baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva, Rich Mavoko (wa kwanza kutoka kushoto), Linah,Barnaba, Joh Makini wakiwa kwenye pozi na mmoja wa mashabiki wao ndani ya Ukumbi wa Escape One katika shoo ya Usiku wa Ishi Kistaa iliyofanyika usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa Hip Hop, Izzo Business akisaini kwenye moja ya bango la shoo hiyo muda mfupi baada ya kuwasili mahali hapo.
Mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo (kulia), akiitangaza shoo hiyo wakati wa kuanza burudani hizo, pembeni yake alikuwa na muongozaji mwenzake wa shoo hiyo, Penny.
Msanii wa Bongo Fleva, Baba Levo akiwa kwenye pozi na msanii mwenzake Meninah.
Mbongo Fleva, Shilole (kulia), akipata kilaji na mmoja wa wasanii wachanga kwenye muziki huo, Rubby.

Mkurugenzi wa Masako wa Vodacom, Kelvin Twissa (kushoto), akipiga stori na msanii wa Hip Hop, Nick wa Pili.
Msanii wa Bongo Fleva, Linah akipozi na msanii mwenzake Rubby.

Shilole (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika pozi na baadhi ya mashabiki waliojitokeza kwenye shoo hiyo ndani ya Ukumbi wa Escape One.
Kadja Maumivu akiwa katika pozi na msanii mwenzake Msamy.
Mwigizaji wa Tamthilia ya Mahusiano, Mwinjaku (kushoto) akiwa katika pozi na msanii wa Bongo Fleva, Rubby.
Shilole akiwa katika pozi na shabiki wake.
USIKU wa kuamkia leo kulikuwa na bata mbalimbali zikiendelea katika kumbi za burudani jijini Dar es Salaam, lakini kati ya kumbi zote bata la nguvu lilikuwa ndani ya Ukumbi wa Escape One Mikocheni, jijini Dar es Salaam kwenye shoo ya Usiku wa Ishi Kistaa ambayo iliwakutanisha baadhi ya mashabiki wa burudani na mastaa mbalimbali wa Bongo Fleva na Bongo Movies ambao waliinjoi kwa kucheza muziki mzuri sambamba na mashindano ya hapa na pale.
Miongoni mwa mashindano madogomadogo yaliyoendeshwa na waandaaji wa shoo hiyo ni pamoja na mashabiki kuimba akapela ya wimbo wa msanii yoyote kisha kupatikana mshindi ambaye alitangazwa na burudani ikaendelea.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...