Monday, March 30, 2015

PLATINUM YA YANGA YAZIDI KUPOTEA MABOYA ZIMBABWE

WANAISUBIRIA Yanga? Ni suala la kujiuliza kwa harakaharaka kwa klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe, jana kufungwa kirahisi katika mchezo wa ligi kuu nchini humo, dhidi ya Caps United.
Timu hiyo ilikuwa ugenini ambapo ilikubali kichapo cha
bao 1-0, ukiwa ni mchezo wa raundi ya pili ambapo kichapo hicho kimeifanya kushika nafasi ya 10 na pointi moja, baada ya kutoa sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo. 
Muuaji wa Platinums,  Ronald Pfumbidzai wa Caps
Kichapo hicho kimemuweka kocha wa Platinum, Norman Mapeza, kutokana na matokeo mabaya katika
michezo ya hivi karibuni.
 Duru za michezo kutoka nchini humo zinasema kuwa 
huenda kocha huyo akafungashiwa virago huku 
kichapo cha Yanga kikitajwa kuwa chagizo kuu.

Matajiri hao wa madini, hawajashinda katika michezo mitatu ambapo mkosi ulianzia kwa Yanga, kisha kulazimishwa sare ya mabao 2-2 kabla ya jana Jumapili kula mweleka mbele ya watoto wa mjini, Caps.
Roho mkononi... Kocha wa Platinum Mapeza huyo hatarini kufukuzwa kutokana na matokeo mabaya
Timu hiyo itakwaana na Yanga Jumamosi wikiendi hii, katika mkondo wa pili wa michuano ya Kombe la Shirikisho hatua ya mtoano, lakini Yanga ina faida ya ushindi wa mabao 5-1, hivyo Platinum inahitaji ushindi wa mabao 4-0.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...