Friday, March 27, 2015

LADY JAYDEE AJICHAGULIA JENEZA

Uchuro? Baada ya kutundika mtandaoni kwa mara nyingine picha za jeneza alilojiandalia litakalotumika siku akiaga dunia, mwanamuziki Judith Daines Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee au Jide, amelaaniwa vikali na mashabiki wake kwa kitendo hicho.
Mwanamuziki Judith Daines Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee au Jide.
ABADILI RANGI
Mwaka 2012, Jide alitupia mtandaoni picha za jeneza lake lenye mchanganyiko wa rangi ya zambarau na nyeupe lakini safari hii amebadilisha na kutupia mengine mawili yenye rangi ya krimu na nyeupe.
MANENO KUNTU
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo anatumia jina la jidejaydee, juzi, mwanadada huyo, pamoja na picha hizo mbili, alisindikiza na maneno kuntu kwa chini yaliyosomeka, ‘Nimebadilisha mawazo yangu, sitaki tena lile la zambarau. Moja kati ya hayo hapo juu. Msinimaindi. Kila mtu atakufa. Nilikuwa nafikiria pia iwe kwa waalikwa tu. Sitaki kufunuliwa’.
MASHABIKI WAMLAANI
Risasi Jumamosi liliinyaka ishu hiyo sekunde chache baada ya Jide kuitupia ambapo ndani ya muda mfupi ‘posti’ hiyo ilikuwa na maoni mengi ya kulaani kitendo hicho.
Baadhi ya mashabiki walieleza waziwazi kuchukizwa na jambo hilo alilolifanya staa wao wanayempenda.
SEHEMU YA MAONI
“Kifo kipo kwa kila binadamu lakini hatutakiwi kukifikiria hivyo dada (Jide) unamkosea muumba wako.
“Wewe ni kioo changu, ila kwa hili kwa kweli sijalipenda.
“Jamani dada mbona unatutisha au haupo sawa leo?
“Wewe wajina umefikiria nini lakini?
“Kama umeshaona unakufa sema tujue.
Muonekano wa jeneza hilo.
“Duh! Dada fanya maombi hiyo ni roho ya umauti.
“Dada nini tena mbona unamkufuru Mungu?                      Hata kama una machungu kiasi gani, huwezi kufanya hivyo kwani ni mipango ya Mungu. Muombe akusamehe.
“Wewe Jide wewe huogopi lakini?
“Najua sote tupo njia hiyo lakini kwa nini leo umeamua kutuandikia hivyo? Naomba mipango ya shetani ishindwe!” ilisomeka sehemu ya maoni hayo iliyoungwa mkono na baadhi ya mashabiki wake waliojawa na simanzi.
MCHUNGAJI AMUUNGA MKONO
Akizungumzia tukio hilo, mchungaji maarufu jijini Dar alisema kuwa, kila mtu anatakiwa kujiandaa kwa kuwa kila nafsi itaonja umauti hivyo ni vema kujiandaa kwa kutenda mema.“Maandalizi yanayopaswa kuwa makubwa ni ya kiroho kwa kuhakikisha unatenda mema ili kupata tiketi ya kwenda peponi na kukwepa adhabu ya Jehanamu,” alisema mchungaji huyo.
KUTOKA RISASI JUMAMOSI
Kifo ni haki yetu lakini si vema kumchuria mtu au kujichuria kwa kuwa ni tukio lisilozoeleka katika maisha ya mwanadamu.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...