Sunday, March 22, 2015

NI LIVERPOOL VS MANCHESTER UNITED LEO

MECHI ya kukata na shoka kati ya Liverpool na Manchester United itapigwa leo kwenye Uwanja wa Anfield jijini Liverpool, England kuanzia saa 10:30 jioni.
Mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge.
Timu hizi mbili ndizo zilizopata umaarufu mkubwa nchini England ambapo Liverpool imetwaa taji la Ligi Kuu ya England mara 18 huku Manchester United wakilitwaa mara 20.
Nahodha na mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.
Katika Ligi Kuu ya England, timu hizo zimekutana mara 163, kati ya hizo Man United wameshinda michezo 64, Liverpool wakishinda 55 na kutoka sare michezo 44.
Mechi ya leo itakuwa na presha kubwa kutokana na kila timu kuwania kukaa katika nafasi za juu kwenye ligi hiyo yenye ushindani mkubwa.
Kwa sasa Manchester United wana pointi 56 wakiwa nafasi ya nne huku Liverpool wakiwa nafasi ya tano wakiwa na pointi 54 wakitofautiana kwa pointi mbili tu.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...