Tuesday, March 24, 2015

LULU MASOMO YAMZUIA KUJIRUSHA

STAA wa filamu  Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekiri kuwa ubize wake katika masomo umemzuia kwa kiasi kikubwa kupata muda wa kufikiria mambo ya kijinga na hata kujirusha.
Staa wa filamu  Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akichonga na paparazi wetu juzikati, Lulu alisema mtu akisimamia kwenye masomo hawezi kuwa na mawazo mabovu kama ya kwenda kujirusha au kupata kilevi badala yake unajikuta ukifikiria masomo na mitihani tu.
“Jamani kama mimi sasa hivi sina hata ninachokiwaza zaidi ya masomo yangu na mitihani ninayokutana nayo yaani hata muda wa kusema utaenda Club, hakuna nafasi kabisa katika kichwa, hivyo nimeamini kuwa ukiwa bize na masomo akili za ajabu hazipo kabisa,” alisema Lulu.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...