Monday, March 23, 2015

LINAH AFANYA ‘BETHIDEI’ NDANI YA BOTI


Msanii wa Bongo Fleva, Linah akiwa amezungukwa na baadhi ya ndugu na jamaa zake wakati akikata keki iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya sherehe ya kuzaliwa kwake iliyofanyika ndani ya boti.
Keki ya bethidei ikiwa mezani kabla ya kukatwa.
Linah akimlisha keki kaka’ake.

Baadhi ya misosi iliyokuwa imeandaliwa kwenye sherehe hiyo ikiwa mezani.
Mmoja wa waalikwa akilishwa keki.
Mwandishi wa magazeti ya Global Publishers LTD, Musa Mateja (kushoto), akilishwa keki na Linah.
Mmoja wa watangazaji wa Clouds TV, Jacob Mbuya (kushoto), akilishwa keki na Linah.
Linah (kulia), akilishwa kipande cha keki na mmoja wa marafiki zake.
Linah akiwa katika pozi na wasanii wenzake.
Mtangazaji wa Global TV Online, Shorvieny Mohamed akimfanyia mahojiano Linah kwenye sherehe hiyo.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva wakipata vinywaji kwa pamoja kwenye sherehe hiyo.

Msanii wa Hip Hop, Young Killer (kushoto), akiwa amepozi na msanii mwenzake Edo Boy ndani ya Ukumbi wa Paparazi uliopo ndani ya Hoteli ya Slipway.
Linah akipozi na marafiki zake.
Peter Msechu akikodoleana macho na Linah baada ya kukutana kwenye sherehe hiyo.
Msanii wa Bongo Fleva, Recho (kulia), akiwa katika pozi na marafiki zake kwenye sherehe hiyo.
Mwana FA (wa kwanza kushoto), akiwa katika pozi na Linah, pamoja na Andrew Kusaga.
STAA wa Bongo Fleva, Esterlina Sanga ‘Linah’, juzikati alifanya sherehe ya siku yake ya kuzaliwa (bethidei) ndani ya boti iliyokuwa ndani ya maji ya Bahari ya Hindi, jirani na eneo la Hoteli ya Slipway, Masaki jijini Dar es Salaam.
Wasanii kibao wa muziki wa kizazi kipya walihudhuria sherehe hiyo iliyofana vilivyo.
(HABARI/PICHA: MUSA MATEJA)

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...