Sunday, March 22, 2015

AMINA MWIDAU (VITI MAALUMU CUF) NDIYE MWENYEKITI MPYA WA KAMATI YA PAC


Mwenyekiti mpya wa Kamati ya PAC, Amina Mwidau (Viti Maalumu Mkoa wa Tanga CUF).
MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF) ndiye Mwenyekiti mpya wa Kamati ya PAC baada ya aliyekuwa mwenyekiti wake, Zitto Kabwe kung'atuka kwenye nafasi yake ya ubunge.
Kupitia akaunti yake ya Facebook, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) na Mwenyekiti wa Kamati ya PAC ambaye jana alijiunga rasmi na Chama cha ACT-Tanzania, Zitto Kabwe amempongeza Amina kwa imani aliyopewa na wajumbe wenzake wa Pac.
"Nimefanya kazi na Amina tangu mwaka 2010 tulipokuwa kamati ya POAC na nina imani, kwa ushirikiano mkubwa wa Makamu Mwenyekiti ndugu Deo Filikunjombe wataendeleza kazi tuliyoianza ya kujenga mfumo madhubuti wa Uwajibikaji nchini kwetu" aliandika Zitto Kabwe

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...