Friday, March 13, 2015

KINYAIYA AFUNGUKA MADAI YA KUUZA UNGA

BAADA ya tetesi kuzagaa kwamba Mtangazaji wa Clouds TV, Benny Kinyaiya anafanya biashara haramu ya kuuza madawa ya kulevya ‘unga’ ambapo husafiri mara kwa mara kinyemela kwenda Ulaya, mwenyewe amefungukia tuhuma hizo.
Mtangazaji wa Clouds TV, Benny Kinyaiya.
Akichati na gazeti hili juzi akiwa nchini Uingereza, Benny alisema kuwa anashangazwa na madai hayo kwani hajawahi na wala hafikirii kufanya biashara hiyo.
“Hizo taarifa ni za uongo kabisa, ni kweli nasafiri mara kwa mara na hata sasa niko Ulaya kwa biashara zangu binafsi lakini hilo la unga siyo kweli, ni uzushi tu. Kuna mambo yangu ya kibiashara nakuja kufanya ambayo siwezi kuyaanika,” alisema Benny.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...