Wednesday, March 18, 2015

CHAMA CHA MADAKTARI WA KINYWA NA MENO WAENDELEA KUTOA HUDUMA YA BURE KATIKA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI ALBINO‏


Prof. Bakari Lembaliti ambaye ni Mwalimu wa Chuo Kikuu Muhas Muhimbili akiwapatia miswaki na Dawa watoto wenye ulemavu wa macho baada ya kuwapa elimu ya matumizi ya usafi wa kinywa na meno inayo endelea kwa siku ya pili katika Shule ya Msingi Buhangija iliyopo Shinyanga
Prof. Bakari Lembaliti (kushoto)  ambaye ni Mwalimu wa Chuo Kikuu Muhas Muhimbili akiongea na Mwanafunzi Khassan Shaban ( aliye vaa kofia kulia) anayesoma katika Sekondari ya Muhumbu Islamic ambaye amedhaminiwa na Shirika fulani anakwenda na kurudi katika kituo hicho ambapo analipiwa ada tu na mambo mengine ajitegemea
Mwalimu wa kitua hicho( aliyeka kulia)   ambaye anayehusika naupokeaji wa watoto hao akiendelea kuwapokea watoto hao wanao letwa na wazazi wao kwa kuhofia usalama wa watoto wao, leo amepokea zaidi ya watoto 12 toka sehemu mbalimbali.
Chama cha Madaktari ,wameendelea kutoa huduma hiyo hata kwa watu wazima waliofika kufanyiwa usafi wa Kinywa na Meno, mwanadada akiwa amezibwa meno baada ya kuonekana yametoboka Meno yake.
Raisi Mstaafu wa Chama cha  Madaktari wa Kinywa na Meno na Daktari Bingwa wa Watoto  Rachel Mhavile  toka Hospitali ya Taifa  Muhimbili, akifanya ukaguzi wa kinywa na Meno kwa Kuyela Masuka, aliyeanguka toka juu ya mti nakusababisha jino lake lambele juu kushotolikawa linaninginia na kunadaktari aliye jaribu kulirudishia lakini tiba hiyo ikamshinda kwa sababu hakua amepiga mswaki vuzuri na kumsababishia kupata maambukizi na kushindwa kufumba mdomo na kutokula chakula, matibabu aliyoyapata toka kwa Daktari Bingwa huyo ni kung'olewa jino na baadaye watampeleka Hospitali ya Mkoa kupiga X-rey kuhakikisha Meno ya jirani yaliyotumbukia kwenye Mifupa hayata athiri.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...