Tuesday, March 24, 2015

ANGELINA JOLIE AFANYIWA UPASUAJI, ATOLEWA OVARI, MIRIJA YA UZAZI

Angelina Jolie.
MWIGIZAJI wa filamu nchini Marekani, Angelina Jolie amelazimika kutoa ovari zake pamoja na mirija ya uzazi baada ya uchunguzi kuonesha kuwa alikuwa katika hatari ya kuathirika na saratani ya nyumba ya uzazi.
Angelina Jolie, mumewe Brad Pitt wakiwa na watoto wao.
Staa huyo maarufu wa Hollywood amelidokezea jarida la New York Times, kuwa alilazimika kutoa viungo hivyo wiki iliyopita katika upasuaji wa dharura.
"Upasuaji huo ulitokana na ripoti ya uchunguzi wa daktari uliobaini kuwa nilikuwa na asilimia 50 ya chembechembe zenye hatari ya kuambukizwa saratani" alisema Jolie
Habari hizi zimewashtua mashabiki wa mrembo huyo ambaye miaka miwili iliyopita alilazimika kukatwa titi kwa sababu ya tishio hilo hilo la Saratani.

Angelina Jolie akiwa na mumewe Brad Pitt.
Mama mzazi wa staa huyo aliaga dunia kufuatia hitilafu iliyotokana na matibabu ya saratani.
"Siyo jambo rahisi sana kukabiliana na swala hili gumu linalohusu afya yangu" aliongeza Jolie.
Jolie ambaye ni mke wa mwigizaji nyota wa Holywood, Brad Pitt, anasema kuwa vipimo vilionesha chembechembe za maradhi hayo na ikamlazimu kuchukua hatua hiyo mara moja.
Mastaa hao wana watoto sita ambapo kati yao wengine ni wakuhasili.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...