Tuesday, February 10, 2015

YANGA YAKUBALI KULIPA MAMILIONI YA NGASSA, ILA KWA SHARTI ZITO

Mkuu wa Idara ya Habari wa Yanga (katikati), Jerry Murro akisitiza jambo katika mkutano na wanahabari leo kwenye Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani.

Ngassa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) akifafanua kuhusu deni linalomtesa. Kushoto ni mkuu wa idara ya habari, Jerry Murro.

Yanga imesema ipo tayari kusimamia deni la zaidi ya milioni 40 anazodaiwa na Benki ya CRDB alilokopa kwa ajili ya kulipa faini aliyopigwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kosa la kusaini mkataba katika klabuni mbili; Simba na Yanga ambapo alitakiwa kuilipa Simba, lakini ikasema kuwa lazima kutakuwa na masharti ya kufuata ili kuhakikisha kiasi hicho anakirejesha.
Deni hilo limemtesa sana mchezaji huyo na kumtoa kwenye mudi ya kucheza soka, kutokana na benki kumkata mamilioni ya fedha huku hivi karibuni ikizuia mishahara yake miwili, jambo lililomfanya akose amani ndani ya klabu.
Akizungumza leo kwenye mkutano na wanahabari, Ngassa alisema kuwa kutokana na deni hilo ameamua kuuomba uongozi kumsaidia kulipa deni hilo, ambapo mkuu wa idara ya habari wa klabu hiyo, Jerry Murro
akikiri kumsaidia ndani ya wiki moja.
"Kama uongozi kwa kutambua umuhimu wa Ngassa kama mchezaji wetu, tumeamua kuwa sekretarieti itakaa kuzungumzia ombi lake la kuomba kumsaidia, naahidi tutamsaidia na ndani ya wiki moja suala hilo litakuwa limetafutiwa ufumbuzi. Lakini ikumbukwe kuwa hela yoyote ile ya Yana ni mali ya wananchi, hivyo ni lazima ziwe na utaratibu katika matumizi, vinginevyo tutapigwa mawe. Kwa hiyo tunaahidi kumsaidia lakini tutaangalia ni jinsi gani ya kuweza kurudisha kiasi hicho,” alisema Murro.
Kwa upande wa Ngassa, alifunguka kilichomnyima furaha klabuni hapo ambapo alisema: “Ni kweli nikosa raha kutokana na makato makubwa kwenye deni hilo. Nilikuwa nikikatwa kiasi fulani (laki tano) kwa kila mshahara, lakini mshahara wangu wa miezi miwili sikuiona, iliniuma sana, hivyo nimewaomba viongozi wangu kunisaidia katika hili, na wameniahidi kulifanyia kazi.
“Naamini litakwisha na nitarudi katika kiwango changu na nina uhakika ninaweza kuwa haa mfungaji bora kama nilivyofanya msimu ulioisha nilivyokuwa mfungaji bora wa Afrika kwenye michuano ya Shirikisho na mfungaji bora wa klabu,” alisema nyota huyo wa zamani wa Simba, Kagera na Azam.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...