Friday, February 6, 2015

SOMA HAPA KUJUA UTATA WA MTOTO WA FLORA MBASHA


Mwimba Injili nyota nchini, Flora Henry Mayalla Mbasha akiwa na mtoto wake wa kike baada ya kujifungua.

Stori:MWandishi wetu

HAKUNA jambo dogo! Siku tano zimekatika baada ya mwimba Injili nyota nchini, Flora Henry Mayalla Mbasha kujifungua mtoto wa kike huku kichanga hicho kikiibua mazito kwenye mitandao ya kijamii, Ijumaa ‘Kubwa’ linakupa zaidi.
Kwa mujibu wa chanzo, Flora alijifungua mtoto wa kike kwa njia ya upasuaji Jumanne iliyopita kwenye hospitali moja iliyopo jijini Dar es Salaam.
MSHTUKO KWANZA
Baadhi ya mitandao ya kijamii ilitundika picha ya Flora akiwa kitandani hospitalini na kichanga chake huku watu wakitupia maneno yenye kuonesha mshtuko, kama vile:
“He! Kwani Flora alikuwa na mimba? Mbona alikuwa kawaida sana?”
“Wanawake wengine wameumbwa hivyo, matumbo yao hayawi makubwa. Nampa hongera kwa kujifungua.”
“He! Jamani! Dada Flora kajifungua kweli au ni igizo? Maana isijekuwa sinema halafu tukampa hongera za bure tu.”
Mtoto anayedaiwa kuibuwa mazito.

‘UTABIRI’ WAANZA
Kama ilivyo kawaida kwa baadhi ya mitandao ya kijamii Bongo. Kusema chochote bila kusikia kauli ya mhusika, baadhi ya mitandao ikaanza kupitisha mitazamo kwamba, mtoto huyo amefanana na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
KIGEZO
Kigezo walichotumia watu hao ni ule mgogoro kati ya Flora Mbasha na mumewe, Emmanuel Mbasha miezi saba iliyopita ambapo Flora aliondoka kwa mumewe, Tabata na kudaiwa kuishi kwa Gwajima.
MPAKA PICHA
Baadhi ya mitandao ilipitiliza kwa kutundika picha ya Gwajima akiwa ameshika kipaza sauti sanjari na ya mtoto huyo akiwa ndani ya ‘bebi shoo’
IJUMAA LAZUNGUMZA NA FLORA
Baada ya kutokea kwa hali hiyo ndani ya mitandao, Ijumaa lilimsaka Flora kwa njia ya simu ili kujua ukweli wa yeye kujifungua mtoto na pia kumtaja baba wa mtoto.
Ijumaa: “Mambo Flora? Hongera kwa kujifungua.”
Flora: “Asante sana.”
Ijumaa: “Kumbe umejifungua bwana!”
Flora: ”Mbona umechelewa kujua!”
Ijumaa: “Mtoto gani?”
Flora: “Wa kike.
MBASHA APIGA CHENGA
Ijumaa liliamua kumuuliza Flora kama mumewe, Mbasha ameshafika kumuona mtoto huyo.
Ijumaa: “Oke! Mungu amtunze na kumsimamia katika afya njema. Vipi baba yake (Emmanuel) ameshakuja kumuona?”
Flora: “Hajaja. Lakini it’s ok! Maana Mungu mwenyewe atamlea.”
MADAI ETI NI WA GWAJIMA
Ijumaa: “Sasa baadhi ya watu wameanza kusemasema eti ni mtoto wa Gwajima. Watu bwana!”
Flora: “Acha tu waseme lakini uzuri mtoto kamfanana baba yake (Emmanuel) kwa kila kitu. Wanaosema kuhusu Gwajima wana lao jambo na hawajui walisemalo.”
ANENA MAZITO
Ijumaa: “Nashukuru sana Flora.”
Flora: “Asante na wewe, lakini narudia tena, wanaosema ni mtoto wa Gwajima Mungu na awabariki tu maana mimi sitishwi na maneno ya wakosaji. Namwangalia Mungu tu aliyeniumba na kunifanya niwe hivi nilivyo leo.
“Isitoshe picha walizoeneza mitandaoni si za mwanangu, so hata sipati shida. Biblia inasema pande zote twadhikika bali hatusongwi, twaona shaka bali hatukati tamaa, twaudhiwa bali hatuachwi, twatupwa chini bali hatuangamizwi.
“Kwa hiyo hatulegei bali ijapokuwa utu wetu wa nje umechakaa lakini ndani wafanywa upya siku kwa siku.”
KUMBE PICHA SI ZA MTOTO WAKE
Flora alisema anachomshukuru Mungu picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimwonesha mtoto kama wa siku kumi si za mtoto wake.
Flora: “Kwanza hiyo picha iliyosambaa kwenye mitandao namshukuru Mungu si ya mtoto wangu. Mimi nimeshawasamehe wote walio kinyume na mimi na wale wasioujua ukweli lakini wanasambaza taarifa.”
Ijumaa: “Asante sana Flora.”
Flora: “Nashukuru sana.”
MBASHA HAPOKEI SIMU, SI KAWAIDA YAKE
Baada ya kumaliza kuwasiliana na Flora, Ijumaa lilimpigia simu Emmanuel Mbasha ili kumsikia anasemaje kuhusu ujio wa mtoto huyo hasa ikizingatiwa kwamba, mkewe aliondoka nyumbani kwa muda mrefu.
Simu ya Mbasha iliita bila kupokelewa hata ilipopigwa mara kadhaa jambo ambalo si kawaida yake. Hata pale alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, Mbasha hakujibu kitu!
GWAJIMA KAMA MBASHA TU
Baada ya ukimya wa Mbasha, Ijumaa lilimtafuta Gwajima kwa njia ya simu yake ya mkononi, naye iliita kwa mara kadhaa bila kupokelewa. Lengo la kumtafuta Gwajina ni kutaka kumsikia anasemaje juu ya madai ya watu mtandaoni kudai mtoto ni wake na nini kauli yake dhidi ya watu hao.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...